Hasheem Thabeet afanya kufuru, amwaga mamilioni disco!

Hasheem Thabeet afanya kufuru, amwaga mamilioni disco!

Hebu tujikumbushe na hii list kidogo, alikuwa mbele ya Steph Curry na Harden......anyway kwa wanaotaka kujua Thabeet siku hizi anacheza basketball China

2009 NBA DRAFT ORDER
  • Clippers. Blake Griffin. PF.
  • Grizzlies. Hasheem Thabeet. C.
  • Thunder. James Harden. SG.
  • Kings. Tyreke Evans. PG.
  • Timberwolves. Ricky Rubio. PG.
  • Timberwolves. Jonny Flynn. PG.
  • Warriors. Stephen Curry. PG.
  • Knicks. Jordan Hill. PF.
 
Mimi nikiwa kama mdau wa viwanja vya starehe vya usiku, nimekuwa nikikutana na supastaa wa Tanzania, Hasheem Thabeet, ambaye anacheza mpira wa kikapu wa kulipwa huko Marekani.
Wadau wa Arusha wanasema wiki iliyopita Thabeet alikuwa huko siku ya Alhamisi kwenye club inayoitwa Vai Vai. Hapo alionekana akiambatana na crew (wapambe) kibao na kununua vinywaji huku akiwa amezungukwa na vimwana kibao.

Kali kuliko yote ilitokea hivi karibuni siku ya jumapili ambapo mwanamuziki wa Bongo fleva, Dully Sykes, alikuwa anafanya show Bilicanas jijini Dar.
Wakati Dully anaimba wimbo wake maarufu wa "Bongo Fleva Naipenda" jukwaani, Thabeet alienda na kumpa bulungutu kubwa la pesa ambalo ni kati ya shilingi laki 5 mpaka sh milioni 1. Baada ya hapo Dully alipata kiwewe cha ghafla na kuacha kupiga shoo kwa muda huku akimwaga misifa kwa Thabeet.

Thabeet hakuishia hapo, alipanda juu pale Bils na kumwaga mamilioni ya noti chini kwa watu walio kwenye dance floor. Ilibidi watu waache kucheza disco na kuanza kugombania kuokota noti alizokuwa akimwaga. It was raining money...
Pia alizunguka kwenye meza za watu na kuanza kugawa ofa za vinywaji. Wapambe wake wanasema siku hiyo Thabeet alienda Bureau de change na kubadili dola elfu 15 (sawa na shilingi 22.5 milioni). Mpambe huyo alisikika akisema usiku huo mmoja Thabeet aligawa shilingi milioni 10 hapo Bils.

Ukiacha Bils, Thabeet pia amekuwa akitembelea viwanja vingine vya dar karibu kila usiku ikiwemo Nyumbani Lounge kwa Lady JD na Mafian kwa Kimbau. Huko amekuwa na tabia ya kuingia nyuma ya counter na ku-serve vinywaji kwa wateja bure yeye mwenyewe na bili yote hulipa yeye. Alionekana akifanya kufuru hizo huku akiwa ameambatana na girlfriend wake, Jokate.

Pia Thabeet anajulikana kupendelea kwenda Nairobi na wapambe wake na kufanya starehe kubwa. Supastaa huyu akiwa Dar hufikia Kempinski Hotel na kuwaambia wasichana warembo waende kulala naye kwenye hoteli hiyo. Tangu ashushwe daraja kutoka NBA kwenda ligi ya chini, Thabeet amekuwa akionekana mara kwa mara Dar utafikiri hana kazi ya kufanya kule Marekani.
Wadau wanasema kushushwa kwake daraja kunatokana na kushuka kiwango kwa kukosa discipline (nidhamu) ya mazoezi na work ethic.

Afisa mmoja wa Benki iliyopo Dar amesema kuwa Thabeet kwa wiki anapokea zaidi ya shilingi milioni 100 kutoka Marekani na huenda pesa hizo ndiyo zinamchanganya. Ikumbukwe pia kuna siku Thabeet alimpiga mtama mwanamuziki TID nje ya ukumbi wa disco.

Sijui kwa mwenendo huu kijana huyu atadumu mpaka lini kama professional baller huko Marekani. Namuonea huruma kijana huyu, sijui pesa zake anaziwekeza kwenye miradi ya kumsaidia baadaye au la? Maana kashashushwa daraja. Akishindwa huko pia akafukuzwa hali itakuwa mbaya sana kwake.

Mama yake, ndugu zake na marafiki zake wanahitaji kumpatia ushauri wa nasaha.
Limebaki jina tu
 
Hebu tujikumbushe na hii list kidogo, alikuwa mbele ya Steph Curry na Harden......anyway kwa wanaotaka kujua Thabeet siku hizi anacheza basketball China

2009 NBA DRAFT ORDER
  • Clippers. Blake Griffin. PF.
  • Grizzlies. Hasheem Thabeet. C.
  • Thunder. James Harden. SG.
  • Kings. Tyreke Evans. PG.
  • Timberwolves. Ricky Rubio. PG.
  • Timberwolves. Jonny Flynn. PG.
  • Warriors. Stephen Curry. PG.
  • Knicks. Jordan Hill. PF.
Inasikitisha sana maisha kama gwaride ukisema nyuma geuka wa mwisho anakuwa wa kwanza ,leo Stephen curry ni bilionea ,anampunga wa hatari huku TOLU akitambaa na besela.
 
T
Natamani kama angelipata muda wa kusoma ulichokiandika kwa wakati ule miaka zaidi ya 10 iliyopita. Ulikuwa ushauri wenye kila kitu, kuonya wapi atateleza na kupendekeza suluhisho. Kwa mara ya kwanza naona JF comment iliyokuja kuwa utabiri uliotimia. Wakubwa ni wakubwa tu, wameshaona mengi wasikilizwe wanaposhauri na uzuri ni kwamba ulikuwa huko huko USA so ulikuwa ukishauri sio kwa kubabia bali kwa uzoefu halisi wa huko.
Maskini ya Mungu, tall yule tuliyemtegemea aipaishe nchi kamataifa hakuweza hata kumiliki ndondo cup ya Basketball hapa nyumbani. Aione Samatta
 
Hasheem naona allikuwa mzembe na hakujituma inavyotakiwa na aliposhtuka ilikuwa very late na kuishia kupoteza nafasi yake katika NBA, kuna sehemu nimeona analaumu Memphis Grizzlies' kwa kukosa minutes kitu kilichofanya apoteze uwezo wake lakini nafikiri ni BS excuse, NBA hata kama hupati minutes lazima uwe tayari maana kila mtu ni star, hata ukipewa dakika mbili you have to show something, kwa thabeet ilikuwa tofauti performance ilishuka sana, alienda Asia akachezea league za Japan na Taiwan na sasa yuko China, he is still playing at high level lakini sio mpunga mrefu kama NBA, alifanikiwa kuwa MVP Taiwan na kuwa best defender league ya Japan na hata ukiomuona sasa his body is massive like real NBA star, i wish angeweka efforts alizoweka league za Asia akiwa NBA nina uhakika angefanikiwa sana, all in all hii ni lesson unapopewa opportunity ichukue and work hard and NO excuses
 
Back
Top Bottom