Hasheem Thabeet: no longer a Grizzlies' Player!

Hasheem Thabeet: no longer a Grizzlies' Player!

TANMO

JF-Expert Member
Joined
Apr 12, 2008
Posts
11,763
Reaction score
11,873
Mtanzania wa kwanza kucheza katika ligi ya NBA,Hasheem Thabeet aliyekuwa akichezea timu ya Memphis Grizzlies, anatarajiwa kwenda timu ya Houston Rockets ya jijini Houston,Texas katika mabadilishano maalumu baina ya timu hizo mbili.

Katika mabadilishano hayo,mchezaji Shane Battier aliyekuwa akichezea timu anayokwenda Hasheem(Houston Rockets) anajiunga na Memphis Grizzlies.

Maendeleo ya Hasheem katika ligi hiyo ya NBA yamekuwa hayaridhishi. Ana kiwango cha vikapu 1.2 na rebound 1.7 kwa kila mchezo. Hicho ni kiwango cha chini sana kwa mchezaji ambaye alichaguliwa akiwa kama 2nd pick katika draft mwaka 2009.Aliyekuwa 1st pick katika mwaka huo ni Blake Griffin aliyekwenda Los Angeles Clippers.​

Source: BongoCelebrity

My Take:
Ng'ombe wa masikini hazai, au msiba wa kujitakia hauna kilio?
 
Hilo ndo tatizo la wa tz kuridhika kidogo tu kwishney!

Haya sasa inakula kwake
 
Lakini nafikiri kocha wa Grizzlies naye alishindwa kumtumia Hasheem, haiwezekani timu kama Houston Rockets ambayo ina reputation kuubwa tu NBA wakubali kubadilishana kwa 'reject', nadhani kocha wa Houston ameona anaweza kumtumia vipi Hasheem...and we (Tanzanians) can only wish him luck, hoping that he will make us proud!
 
Kweli kocha wa Grizillies ameshindwa kumtumia kabisa HT.

Ila HT nae amekua mvivu sana na mpenda starehe na matanuzi. Inabidi akaze na kukomaa sana na matizi.

Let's hope kocha wa Rockets ataweza kumtumia HT vizuri.
 
bado kijana na bado ana nguvu pambana tu mdogo wangu, amtafute Mutombo huko Houston ampe maujanja na pia tafuta stories kuhusu Ben Wallace
 
Lakini nafikiri kocha wa Grizzlies naye alishindwa kumtumia Hasheem, haiwezekani timu kama Houston Rockets ambayo ina reputation kuubwa tu NBA wakubali kubadilishana kwa 'reject', nadhani kocha wa Houston ameona anaweza kumtumia vipi Hasheem...and we (Tanzanians) can only wish him luck, hoping that he will make us proud!
LOVE IT!kee it up Hasheem you carrying our National Flag
 
Back
Top Bottom