Thabeet anaweza kuja kuwa na off-court issues siku zake za NBA . (Kwa wasiofuatilia michezo na dynamics za professional athletics za Marekani, off-court issues refers to matatizo tatizo yanayo purukusa, yanayo distract timu na mchezaji, hasa mienendo inayohusu public antics and misbehavior.)
On at least two different occasions Thabeet amejiingiza kwenye viugomvi ugomvi kwenye vilabu feki, tena vya wakenya vya East Coast. Kiugomvi kimoja ni Thabeet mwenyewe alikinunua, jamaa wanapigana vikumbo kuhusu demu, Thabeet somehow gets in the middle of it na kuanza kusema "you know who I am...you know who I am?" Scuffle ikafikia ku "take it outside," lakini zikaamuliwa kabla wazee hawajaitwa.
Mi nikawaza, Thabeet, you have a bright and promising future ahead of you, kwa nini unataka kuanza na vi rekodi vibaya vibaya na law enforcement saa hizi kwenye vi night spots havina hata fire alarm batteries?
Wamarekani, kinyume na wanavyooneka watu wahuni na wenye tamaduni zilizooza, sio decadent and indulgent kihivyo, bado ni watu conservative sana sana. (Inawezekana hata wana maadili kushinda sisi, na ndio maana huwezi kuwa na nyumba ndogo Marekani na ukawa kiongozi.)
In any event, because of such deep conservatism that permeates even into sports culture, hata wanamichezo hawatakiwi kuwa na, sio tu criminal records tu, bali hata police contact!! Ukipigiwa hodi na polisi tu, itaiingia magazetini halafu wanasema una purukusa timu.
Thabeet inabidi aliangalie sana hili. Sasa hivi yuko under tremendous peer pressure ya ku conform to that hip hop, get-outta-ma-face machismo, pressure ambayo ni wengi tu ilitu weigh down. Mpaka baadae ndio unakuja kugundua, you know what, I don't have to be a nigger to be cool. So, naelewa what he is going through, and the pressure will, in fact, intensify once he gets the power of mullah!!
Sasa mara nyingi usipomwimbia nyimbo za pambio mtu fulani prominent unaonekana kama una kikorosho kikorosho hivi. Kumbe nia yako ni kueleza ya kujenga tu.
Lakini Thabeet mwenyewe akisoma hapa anajua what I'm talking about with those prepubescent scuffles he got himself into in the East Coast. Hao ESPN analysts haya hawayajui. Wao sasa hivi wanaangilia tu his on-court issues. Wabongo wenzie ndio wanajua hivi vi scuffles. So, word to the wise, Thabeet.
Kingine, kuhusu mwenendo na tabia, Thabeet bahati mbaya hajazungukwa na jamii fulani ya watu wazima anaewaogopa. Hana support structure, moral support structure, that is. Ana role na vijana wa kibongo, again, hip-hopping, pant-sagging, colloquial-like-that nigger-wanna be's. Vijana ambao hawawezi kumwambia "Hashimu, Hashimu, sikia Mkuu, unaenda kukutana na Rais wa nchi, vua mkofia huo babu, umepewa audience na Mkuu wa Jamhuri!!!" You know, funika kombe mwanaharamu apite. Hakuna wa kumwambia hayo. Inakuwa kama Kikwete ndo kapewa favor ya audience vile. Unafikiri Nyerere angekubali upuuzi wa watoto kama huo? I mean, kuna wakati ili uwe na mwenendo mzuri inabidi uzungukwe na watu wazima fulani unaowaheshimu kwamba duuuh, hapa nikiliharibu fulani atanionaje. Thabeet hajazungukwa na watu hao Marekani. Wale wazungu, kina Jim Calhoun, kocha wa UCONN, hawajui sana anachofanya weekend. Haya yakianza kupata limelight ya NBA watajua.
Isije ikafika huko halafu ikawa too late.