Hashim a.k.a Dogo yupo wapi?

cyo mdini, but kuna swali linanisumbua hivi kwanini mtu akitoka kwenye ukristo akaingia kwenye uislamu...anapotea kabisa katika ramani....mfano muhamad ally, malcolm x...............
 
Mkuu tuwekee hiyo ngoma ya Shadow in the darkness, kiukweli namkubali sana huyu jamaa.

Verse mbili za kwanza Na korasi zipo kwa lugha ya malikia, so sikuzikariri.
Chukua hii verse ya mwisho ipo kikwetu;

Hivi vitu viko wazi, kama vazi la kahaba,
Nasambaza maradhi, halafu nakupa Siku 7,
Machozi ni haba, Uokozi ni Njozi baba,
Ulimwengu wa Saba, Jehanam ya aina yake,

Kipe kitu kikupe, kikutupe kupe akikunyonya damu kwa hamu,
Kama hujafaham, DOGO mwanaharam,
Kalam inamwaga damu,

Nakuacha mweupe ka' mkorogo,
Chata ka' wagogo,
Wabongo acheni nyodo,
Wote mnakula hongo,

Hivi hii ni Serikali,
Au Sera Kali kwa mbali,
Au sera za mali,

Ni ipi,tafakari, nakufa kiume,
Tunapokwenda pana Zali,
Vichaa wangu walume wananyaka hiyo hali,

Tujitume, Pesa tuchume, kwa mwezi tudake,
Utake usitake, kila mjuba sasa kivyake mifuko itune,
Kama hujipendi njoo nichune, wabongo roho ziume,

Kama hufiki, usijikune,
Hivi inatiki,
Kila siku ya wiki,
Ikipata karatasi, wino hutoka kwa kasi,
Basi nina wasiwasi, kwa haya nawahasi,


Kiu ya Jicho, ulicho nacho ndicho ulicho,
Bongo ni Kama ficho, ya huwezi huchezi na anga,
Tokea '78 wabongo wamefunga mkanda!!
 

mkuu kwel unamkubali hashm had leo mistar ipo kichwani
 

hashimu dogo ni habar nyingine anajua sana huyu mtu duuuh
 
here is a track hommie.listen to the swahili lyrics then picture it with the current social/political tragedy that tanzania is passing through there you get to admit Dogo Hashim ni Mwanaharam.
 
Last edited by a moderator:
Dada umetisha,
 

Dogo Hasheem yupo mjini hapahapa Dar anafanya maujanja mengine ambayo bado yanazunguka maisha yetu..
 
Huwezi kumkosoa kala pina kwa staili yake ya kurap kwani kila mtu ana stail yk ya kurap ipo wazi kama hakuna mwanahiphop wa ukweli tz east afrika kama KAMANDA wangu kala pina @
 
Huwezi kumkosoa kala pina kwa staili yake ya kurap kwani kila mtu ana stail yk ya kurap ipo wazi kama hakuna mwanahiphop wa ukweli tz east afrika kama KAMANDA wangu kala pina @

kalapina mkali ila hatii maguu kwa hashim dogo,ni wangu mtazamo tu
 
kwa mnao taka mp3 zake mm nmechukua tubidy.mobi japo zna quality ndogo maana wame convert video kua mp3
 

Tunasonga kwa mwendo wa farasi au kinyonga
 
huyu jamaa alikuwa ni mkali sana, mara ya mwisho nilikutana Libya kabla machafuko ya kumtoa Gaddafi hayajaanza! alikuwa amekuja kikazi na kampuni fulani hivi ya south africa, aliniambia mziki hajaacha bali amepumzika tuu
 
In tha shadow of the dark destiny,
Spark me,
Assess me,
Bless me,
Why u wana be test me,
I'm trying stay sane,
My school of thought reigns,
Let's see who maintains,
And who remains.

Sent from my BlackBerry 9800 using JamiiForums
 
Itachukua miaka mingi kutengeneza kichwa kama Dogo Hashim nchi hii.Jamaa halazimishi game ukiongea nae tu utatambua unaongea na mtu wa aina gani.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…