BARD AI
JF-Expert Member
- Jul 24, 2018
- 3,591
- 8,826
Hashim Rungwe
Mwenyekiti wa Chama cha Ukombozi wa Umma (Chaumma), Hashim Rungwe amesema hakuna sababu ya kwenda kwenye uchaguzi mkuu mwakani bila kuwa na Katiba mpya.
Anasema haamini kama Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi pekee inatosha kuufanya uchaguzi kuwa huru na wa haki kama Katiba haitarekebishwa.
Amesema Katiba mpya ndiyo itamaliza sintofahamu ya upande mmoja kuona uchaguzi hautakuwa huru na haki, licha ya Rais Samia mara kadhaa kuwahakikishia Watanzania kwamba uchaguzi utakuwa huru na wa haki.
“Uchaguzi ujao ufanyike kwa kutumia Katiba mpya, hicho ndicho kitamaliza sintofahamu inayoendelea sasa,” amesema Rungwe katika mahojiano maalumu na Mwananchi yaliyofanyika ofisini kwake, Makumbusho jijini Dar es Salaam hivi karibuni.
Rungwe anasema kama changamoto ya kupatikana kwa Katiba hiyo ni muda, basi vyama vya siasa wakubaliane Rais Samia aongezewe muda, Bunge liridhie, ili muda huo utumike kukamilisha upatikanaji wa Katiba mpya, ndipo uchaguzi ufanyike.
“Kama tatizo ni muda, bora tukubaliane na Bunge liidhinishe Rais aongezewe muda, lakini kwa masharti kwamba katika kipindi hicho kitakachoongezwa tuwe tumepata Katiba mpya, ndipo twende kwenye uchaguzi,” anasema Rungwe.
==============================================
The Chairman of Chama cha Ukombozi wa Umma (CHAUMMA), Hashim Rungwe, has said that there is no reason to go to the general elections next year without a new Constitution.
He believes that the Independent National Electoral Commission alone is not enough to ensure that the elections are free and fair if the Constitution is not amended.
He said that a new Constitution will end the uncertainty of one side thinking that the elections will not be free and fair, despite President Samia assuring Tanzanians several times that the elections will be free and fair.
"The next election should be conducted using a new Constitution, that's what will end the current uncertainty," said Rungwe in a special interview with Mwananchi that took place in his office at Makumbusho in Dar es Salaam recently.
Rungwe suggests that if the challenge is the time it takes to obtain the Constitution, then political parties should agree to extend President Samia's term, and Parliament should approve it, so that the time can be used to complete the process of obtaining a new Constitution before the elections take place.
"If time is the problem, it's better for us to agree and let Parliament approve an extension for President Samia," he said.
PIA SOMA
- Deo Sanga aomba Rais Magufuli aongezewe muda hata asipotaka
- Ally Kessy: Katiba sio msaafu, Rais Magufuli akimaliza muda wake tutatengua Katiba aongezewe muda | Spika Ndugai amuunga mkono
- Mzee Mwinyi: Rais Magufuli aongezewe muda wa miaka 5 zaidi kama shukrani
- Zile kelele za Rais Magufuli aongezewe muda mbona hazipingwi kwa Rais Samia?
- Uchaguzi 2020 - Dkt. Magufuli aongezewe muda wa kutawala
- Rais Magufuli akifanya mambo haya, Watanzania watamlilia wenyewe aongezewe muda wa kutawala
- Kuelekea 2025 - CCM Zanzibar wapendekeza Rais Mwinyi atawale kwa miaka 7, wasema kufanya uchaguzi 2025 ni hasara na matumizi mabaya ya fedha za umma