Pre GE2025 Hashim Rungwe: Tukienda kwenye mikutano ya CCM wanatupa hela, tunazichukua na tutaendelea kuzichukua

Mijadala ya Uchaguzi Mkuu wa Tanzania 2025 (Kabla, wakati na baada)

JanguKamaJangu

JF-Expert Member
Joined
Feb 7, 2022
Posts
2,780
Reaction score
6,607
Your browser is not able to display this video.

Hashim Rungwe ambaye ni Mwenyekiti wa Chama cha Ukombozi wa Umma (CHAUMA) akihojiwa na Edwin Odemba anasema:

“Kila tukienda kwenye mikutano ya vyama vya Siasa CCM inachukua pesa za wananchi inatulipa ili ionekane nchi hii kuna demokrasia, hakuna dawa hosptalini ila pesa za kutulipa wanapata na sisi hatutaacha kuzichukua.”

Chanzo: Star TV
 
Na hata sisi tukienda kwenye mikutano ya CHAUMA, wanatupa ubwabwa, tutaendelea kuubugia na kuufakamia ubwabwa huo vilivyo bila mbambamba yoyote tukingojea bahari isogezwe morogoro 🐒
 
Huo ndo ukweli siasa inalipa saana.kuna wakati huwa naona ata hawa covid 19 wanafanya vizuri kula hela za wananchii wajinga.anayepewa hana kosa mwenye kosa ni mtoaji.
 
Huo ndo ukweli siasa inalipa saana.kuna wakati huwa naona ata hawa covid 19 wanafanya vizuri kula hela za wananchii wajinga.anayepewa hana kosa mwenye kosa ni mtoaji.

..Ccm hawataoi fedha hizo mifukoni mwao.

..Hizo sio fedha binafsi za Mama Abduli, au za Husseni.

..Ccm wanapokea 3.2 BILLION kila mwezi kama ruzuku inayotokana na kodi za Watanzania.

..Mabilioni hayo ndiyo yanayoiwezesha Ccm kufanya vituko na vitimbi vya kila aina ikiwemo kununua magari ya kifahari, mabango ya Mama kila mtaa, na hata kununua wapinzani.
 
'Kula' ni kwa CCM, Ila KURA ziende kwa Wapenda Haki.
 
Pokea maokoto ila kichwani mwako mpe kura mwenye sifa za uongozi, hata kama hajakupa hata senti.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…