Hasira za Pakistan na Iran ni kama za wagonjwa wa safura

Hasira za Pakistan na Iran ni kama za wagonjwa wa safura

Webabu

JF-Expert Member
Joined
Apr 29, 2010
Posts
8,870
Reaction score
14,258
Kwa takriban miaka mitano sana makamanda wakubwa wa Iran na vituo muhimu vya kijeshi vya Iran vimekuwa vikishambuliwa na Israel ndani ya Syria na hata ndani ya Iran yenyewe.

Mtekelezaji wa mashambulio hayo Iran amekuwa akimtaja bila kificho na mwenyewe (Israel) mara moja moja amekuwa akikiri kwamba amehusika.Kinachoshangaza hakuna siku Iran amejibu mapigo kwa Israel.Hata pale alipotoa kitisho kikubwa kwa Israel kuingia Gaza na bado hakufanya chochote.

Kwa upande wa Pakistan nchi ya India ilionesha ubabe mkubwa na kuifedhehesha Pakistan pale ilipojinyakulia jimbo la Kashmir ambalo sehemu mojawapo ilikuwa ni milki ya Pakistan.Kwa jeuri kubwa India ilisema maeneo yote ni ya kwake na ikabadili katiba kutambulisha hivyo.

Wakashmiri wanaofuata uislamu na kujiona ni sehemu ya Pakistan walilia sana lakini bado Pakistan haikuweza kuwasaidia.Kutokea hapo huwa wanavamiwa majujmbani mwao na India na kukamatwa au kuuliwa bila msaada. wowote wa Pakistan.

Wiki mbili ziizopita Iran ikaamua kupiga maeneo iliyosema kuna ofisi za kijasusi ndani ya Pakistan na hata watu wachache raia wa Pakistan wakafa.

Hata siku tatu hazikupita Pakistan ikaamua kupiga maeneo ya Iran na kwa teknolojia kubwa waliyonayo Pakistan wakapatia shabaha pale pale palipokuwa na kamanda mmojawapo wa Iran aliyehusika na kuishambulia Pakistan.

Kwa ujumla hasra za nchi mbili hizi na kukosa subira zinafanana sana na wagonjwa wa safura ambao wakiudhiwa bila kusubiri wanapeleka hasira kwa yeyote aliyekaribu yao.
 
Back
Top Bottom