JanguKamaJangu
JF-Expert Member
- Feb 7, 2022
- 2,780
- 6,607
Kiungo mshambuliaji wa timu ya Simba, Hassan Dilunga ameondoka Nchini Tanzania kuelekea Afrika Kusini kwa ajili ya kupata matibabu ya majeraha yanayomkabili kwa muda mrefu.
Kwa mujibu wa taarifa kutoka katika Klabu ya Simba, imeeleza kuwa nyota huyo ambaye aliwahi kuitumikia Yanga, ameondoka leo Aprili 14, 2022 akielekea Afrika Kusini.
Dilunga maarufu ''HD'' amekuwa nje ya dimba kuwa muda mrefu akiuguza jeraha ambalo limemfanya asiitumikie Simba kwa muda mrefu.
Nyota huyo alijiunga na Simba mwaka 2018 na kuwa sehemu ya mafanikio ya mataji mbalimbali waliyoyatwaa Simba kwa misimu miwili mfululizo.
Source: East Africa TV