Kuna funzo kubwa sana hapa si kwa wachezaji wa mpira tu hata katika maisha ya kawaida ndani ya jamii zetu pale unapoondoka mahali hata kama unaenda sehemu nyingine nzuri kiasi gani usitoe maneno ya kashfa juu ya sehemu unayoondoka. Kwa sababu hatujui ya kesho huenda tukalazimika baadae kurudi pale tulipoondoka mwanzo.
Lakini huyo dogo ana mihemko sana pamoja na kipaji chake. Anapaswa ajiulize mara mbili mbili kwa nini timu zote kubwa zilimkacha wakati anavutana na Yanga? Sio Simba, Azam, Mtibwa wala Singida waliohangaika naye.
Huyo Kesi kuna msimu alisababisha simba ikakosa ubingwa katika mazingira ya kutatanisha sana. Kimsingi wachezaji wetu wanapaswa kujua mpira ni kazi yao wasilete ushabiki wala wasikubali kutumika kuhujumu timu nyingine. Kwani anyekutumia kuhujumu leo kesho akikusajili bado atakosa imani na wewe kuwa unaweza kutumika kuhujumu kama alivyokutumia kuhujumu timu pinzani.
Kimsingi Kesi ajifunze sasa aache utoto, apunguze mihemko na asijione staa kwani bado ana safari ndefu sana. Atulie acheze mpira kwani bado umri unamruhusu kucheza kwa muda mrefu ujao.