Hassan Mwakinyo, bondia anayejiamini katika kazi zake, lazima mzungu akae

Hassan Mwakinyo, bondia anayejiamini katika kazi zake, lazima mzungu akae

Mwishokambi

JF-Expert Member
Joined
Nov 23, 2020
Posts
390
Reaction score
1,425
Aisee tangu nilipoanza kuangalia mchezo wa boxing enzi zile za akina marehemu Stanley Mabesi, Charles Libondo Mawe, Bakary Mambeya, Magoma Shaaban, huku kwenye ridhaa enzi za akina Makoye Isangura, Hassan Matumla, Haji Matumla, Mzonge Rashid nk sijaona bondia anayejiamini na kazi yake kama huyu mdigo mwenzangu Hassan Mwakinyo.

Leo wakati anapima uzito, Mwakinyo hana presha yoyote, unamuona kabisa haogopi kupanda ulingoni licha ya kuwa yuko ugenini, hana kutetemeka na yuko tayari kupiga punch kwa mzungu.

Nina uhakika 90% Mwakinyo anashinda pambano hilo.
 
Mwakinyo alikuwa anawapiga wazungu huko huko bila Tanzania kujua raia wake anapigana na alinyimwa mpaka bendera mpaka mwakiyembe akaingilia kati na leo hii kuna watu wanamchukia mwakinyo licha ya njia alizopitia kweli bongo fanikiwa uchukiwe
Kila la kher mtoto wa tanga wadigo wako pamoja na wewe bila kusahau makorora yote inasimama kesho kumuangalia kijana shujaa wa mtaa wao.
 
Hakuna anayemchukia ila hatoboi
 
Kila lakheri Champez sisi tushatia jamvi apa ukipigwa sawa ukishinda sisi tuvute mpunga maisha yaendelee
IMG_20220903_001753_509.jpg
 
Mimi mdigo mmojawapo.Team Mwakinyo!!

Hassan Mwakinyo ni mdogo sana ila kafikia ndoto za alieanzisha boxing mtaani Makorora, jamaa anaitwa Issa ni marehemu , Issa akawa anahamasisha vijana wa Makorora twende nae Tangamano mazoezi community centre hall!! watu tunajificha tukimuona Issa maana masumbwi si kitoto tulikuwa tunaenda nae Tangamano just for fun ukipigwa ngumi jiwe moja ikajaa vizuri usoni unaona nyota nyota!!kesho wakikuita unalala mbele!!

Marehemu Issa ni ndugu yake na Barua na Tajiri!! Mwakinyo akisoma hii comment atajua hiyo stori!

Watoto wa Makorora na ndoto zetu za kufika majuu!!

All the best Hassan huko uzunguni
 
Natandika mkeka wangu kwa mwakinyo japo najua atoboi,liam smith ni hatari..

Kama namwona mwakinyo kazamia mtumbwi wa kibwengo,kesho atapigwa kama ngoma.

Boxing sio mpira,mwamba atoboi
hivi mitumbwi za vibwengo bado zipo mkuu? niliwahi kusafiria kwenda Pemba.maana niko bize for now sijapata safari ya kwenye maji.
 
Ushindi wa Mwakinyo ni kuvuka round 6 basi.
Liam Smith ni hatari sana.
 
Mnanitisha na nyie mimi nshakandamiza liten langu kwa mwakinyo
 
Back
Top Bottom