Hassan Mwakinyo walitaka nikae kimya ili wanichafue

JanguKamaJangu

JF-Expert Member
Joined
Feb 7, 2022
Posts
2,780
Reaction score
6,607
Akizungumzia pambano lake dhidi ya Bondia Julius Indongo wa Namibia katika kuwania Mkanda wa IBA Intercontinetal, Bondia Hassan Mwakinyo amesema tatizo limeanzia kwa promota ambaye ameenda kinyume na makubaliano yao.

Promota ana rekodi tata
Mwanzoni nilisikia taarifa juu ya Promota, kwamba wana tuhuma za kutowalipa mabondia, baada ya makubaliano tukakubaliana kuwa kazi ifanywe kwa kushirikiana ili kila upande uwe na haki ya kuleta wadhamini.

Kwa maana hiyo nilikuwa na haki ya kuleta mabondia ambao walikuwa upande wangu ili wapigane.

Baadaye Promota akakwama katika suala la fedha, hivyo wakahitaji msaada wa kutoka upande mwingine kitu ambacho ni kinyume na makubaliano yetu kwa kuwa wao walitakiwa kusimama mpaka mwisho.

Baadaye wakaingia mkataba na Promota ambaye sisi (timu ya Mwakinyo) hatuna uhusiano naye mzuri, nikawauliza wakasema hizo taarifa hazina ukweli.

Baadaye nikabaini hakuna ukweli katika mazungumzo yake (Promota), ikabidi nianze kurekodi mazungumzo yetu yote kuhusu tukio hilo.

Promota akasema kuwa alishirikisha kampuni nyingine kwa kuwa fedha ya kulipia mkada haikuwepo, ikabidi mimi ndio nilipie mkanda kwa Dola 4,000.

Mpinzani Mkenya ajitoa
Kuhusu mpinzani wangu wa awali (Rayton Okwiri) nadhani aliambiwa na watu kuwa anaenda kupigana na bondia mkubwa, hivyo akapandisha dau ikashindikana kwake.

Wakatafuta mpinzani mwingine kwa haraka, ofa yake ikawa juu zaidi ya waliyokuwa nayo, tukakubaliana kuwa Promota atoe nusu ya pesa nasi tutoe ili aongezewe bondia mpya.

Ilivyofika siku ya kupima uzito nikawaona watu ambao hawakuwa kwenye mipango yetu, wakadai kuwa baada ya kumaliza vipimo tutazungumza.

Baada ya vipimo hakukuwa na kikao chochote, nikapiga simu naambiwa nimeshauzwa, nifanye ninachotaka.

Promota alinichukulia poa labda kwa kuwa aliona amenizidi umri a hakujua misimamo yangu.

Walitaka wauze tiketi kwa kutumia jina langu, labda walitaka mimi nikae kimya ili niharibikiwe.
 
𝙿𝚛𝚘𝚖𝚘𝚝𝚊 𝚔𝚊𝚝𝚑𝚒𝚋𝚒𝚝𝚒𝚜𝚑𝚊 𝙼𝚠𝚊𝚔𝚒𝚗𝚢𝚘 𝚊𝚗𝚊𝚌𝚑𝚊𝚐𝚞𝚊 𝚖𝚊𝚋𝚘𝚗𝚍𝚒𝚊 𝚗𝚢𝚊𝚗𝚢𝚊 ,𝚠𝚊𝚔𝚒𝚖𝚝𝚊𝚏𝚞𝚝𝚒𝚊 𝚖𝚊𝚋𝚘𝚗𝚍𝚒𝚊 𝚠𝚊 𝚖𝚊𝚊𝚗𝚊 𝚊𝚗𝚊𝚠𝚊𝚔𝚊𝚝𝚊𝚊 𝚑𝚊𝚝𝚊 𝚢𝚞𝚕𝚎 𝚖𝚔𝚎𝚗𝚢𝚊 𝚒𝚕𝚒𝚋𝚒𝚍𝚒 𝚠𝚊𝚋𝚎𝚖𝚋𝚎𝚕𝚎𝚣𝚎 𝚜𝚊𝚗𝚊 𝚌𝚑𝚊𝚖𝚊 𝚌𝚑𝚊 𝚗𝚐𝚞𝚖𝚒 𝚊𝚏𝚛𝚒𝚔𝚊 𝚒𝚕𝚒 𝚔𝚒𝚔𝚞𝚋𝚊𝚛𝚒 𝚊𝚙𝚒𝚐𝚊𝚗𝚎 𝚗𝚊 𝚖𝚠𝚊𝚔𝚒𝚗𝚢𝚘 𝚔𝚠𝚊𝚗𝚒 𝚑𝚊𝚔𝚞𝚠𝚊 𝚗𝚊 𝚜𝚒𝚏𝚊
 
Bongo dalisalama

Sent using Jamii Forums mobile app
 
𝙿𝚛𝚘𝚖𝚘𝚝𝚊 𝚔𝚊𝚝𝚑𝚒𝚋𝚒𝚝𝚒𝚜𝚑𝚊 𝙼𝚠𝚊𝚔𝚒𝚗𝚢𝚘 𝚊𝚗𝚊𝚌𝚑𝚊𝚐𝚞𝚊 𝚖𝚊𝚋𝚘𝚗𝚍𝚒𝚊 𝚗𝚢𝚊𝚗𝚢𝚊 ,𝚠𝚊𝚔𝚒𝚖𝚝𝚊𝚏𝚞𝚝𝚒𝚊 𝚖𝚊𝚋𝚘𝚗𝚍𝚒𝚊 𝚠𝚊 𝚖𝚊𝚊𝚗𝚊 𝚊𝚗𝚊𝚠𝚊𝚔𝚊𝚝𝚊𝚊 𝚑𝚊𝚝𝚊 𝚢𝚞𝚕𝚎 𝚖𝚔𝚎𝚗𝚢𝚊 𝚒𝚕𝚒𝚋𝚒𝚍𝚒 𝚠𝚊𝚋𝚎𝚖𝚋𝚎𝚕𝚎𝚣𝚎 𝚜𝚊𝚗𝚊 𝚌𝚑𝚊𝚖𝚊 𝚌𝚑𝚊 𝚗𝚐𝚞𝚖𝚒 𝚊𝚏𝚛𝚒𝚔𝚊 𝚒𝚕𝚒 𝚔𝚒𝚔𝚞𝚋𝚊𝚛𝚒 𝚊𝚙𝚒𝚐𝚊𝚗𝚎 𝚗𝚊 𝚖𝚠𝚊𝚔𝚒𝚗𝚢𝚘 𝚔𝚠𝚊𝚗𝚒 𝚑𝚊𝚔𝚞𝚠𝚊 𝚗𝚊 𝚜𝚒𝚏𝚊
Hata Mimi nimemsikiliza vizuri, mwakinyo kazingua kwenye hili.

Sent from my Infinix X6511B using JamiiForums mobile app
 
Huyu jamaa siku hizi anatrend zaidi kwa porojo kuliko kazi yake ulingoni. Yuko na "big fat ego" pamoja na ulimbukeni mwingi.

Asipokua makini, anaweza kujichimbia shimo ambalo hataweza kutokamo!
 
Back
Top Bottom