Inasemekana Ruge Mutahaba kaamua kumrudisha haraka ' Jamaa ' hasa baada ya ' mkwara ' wa Mange Kimambi kwamba kwanini hapendi Watangazaji wake wamjadili / wamzungumzie Tundu Lissu. Inadaiwa kwamba kama leo ' Mtangazaji ' huyu asingesamehewa na kurudishwa ' Kundini ' basi Mwanadada ' Mghaibuni Mpinzani ' Mange Kimambi kuanzia leo alikuwa anaenda kutiririka na kuserereka na ' maovu ' kibao ya aibu ya Ruge Mutahaba ambayo pengine yangeweza hata kumuharibia ' career ' yake.
Pengine kwakuwa ' biti ' la Mange Kimambi ( Mghaibuni Mpinzani ) limeweza kufanikisha Yeye ( Hassan Ngoma ) kurudishwa ' Kundini ' labda ndiyo maana ' Jamaa ' nae kaamua ' Kujibatiza ' upya na kujiita Hassan Ngoma Mange Kimambi Dotto Bahemu.
Sasa Kazi imeanza na ndiyo Kumekucha. Mnaomfolo Mange Kimambi si vibaya mkatuambia baada ya leo Hassan Ngoma kuonekana akiwa katika Kipindi akiwajibika tena vizuri tu Yeye anasemaje au ana maoni gani. Je atawaombeni msahama aliwaowalisha ' matango pori ' yake au labda atakuwa na mapya zaidi?