GE2025 Hasunga aahidi kuleta magari mawili kusaidia misiba akichaguliwa jimbo la Vwawa

Matukio, Taarifa, Habari na Mijadala ya Wananchi WAKATI wa Mchakato wa Uchaguzi Mkuu 2025

DuaZaMama

JF-Expert Member
Joined
Jun 2, 2025
Posts
1,882
Reaction score
4,153
MGOMBEA ubunge wa Jimbo la Vwawa kupitia Chama Cha Mapinduzi (CCM), Japhet Hasunga, amesema akichaguliwa ataendelea kutoa huduma ya gari la kusafirisha miili ya marehemu wanaofariki dunia ndani ya jimbo lake ili kuwapunguzia gharama wafiwa.

Aidha Hasunga amesema akichaguliwa tena ataongeza gari la pili ili yawe mawili na yafanye kazi hiyo kwa ufanisi zaidi.

Amesema hayo Septemba 11 alipokuwa akiomba kura katika Kata ya Isalalo ambapo amewaomba wakazi wa kata hiyo wenye vitambulisho vya mpiga kura kuwapigia kura wagombea wote wa CCM siku ya Oktoba 29 mwaka huu.

Hasunga amewaomba wapiga kura wajiandae kumpigia kura mgombea wa urais kupitia CCM Samia Suluhu Hassan, mgombea Ubunge kupitia CCM, Japheti Hasunga na Mgombea Udiwani kupitia CCM kata ya Isalalo Happy Msokwa.

Kwa mujibu wa dereva wa gari linalosaidia kusafirisha miili ya marehemu Daud Mwambene wastani wa mwili mmoja umebebwa kila siku na kwamba siku nyingine alibeba miili hadi mitatu kwa siku.

Kuhusu ubebaji wa wagonjwa kutoka Zahanati au vituo vya afya kwenda hospitali kubwa amesema Serikali ya CCM imeleta magari matano kwenye jimbo lake ambayo yanafanya kazi kwenye vituo vya afya wakati wowote yanapoitwa.
1757679449353.png
 
Ccm inajali sana misiba, wanaweza wasitatue shida iliyosababisha misiba ila wapo tayaru kuendesha mazishi ya kimkoa au wilaya
Mwaka huu una maneno, nilisikia vile vile ati kero kubwa ya uchaguzi ni watu kushindwa kuchukua wafu wao toka mahospitalini kwa maziko.
Really?
Hili ni la kuongelewa kama kero katika kampeni ya uchaguzi?
Pathetically low minded!
 
  • Thanks
Reactions: Lax
Huyu mwehu kweli, wananchi wanataka dawa mahospitalini ili wapone waendelee na kazi zao. Yeye anawaza wafe ili awasafirishe..!!

Km vipi awaombe hizo kura marehemu wanaotaka kusafirishwa..!!
 
Mwaka huu una maneno, nilisikia vile vile ati kero kubwa ya uchaguzi ni watu kushindwa kuchukua wafu wao toka mahospitalini kwa maziko.
Really?
Hili ni la kuongelewa kama kero katika kampeni ya uchaguzi?
Pathetically low minded!
HIki chsms hata yakitokea majanga wapo focused sana na mazishi
 
MGOMBEA ubunge wa Jimbo la Vwawa kupitia Chama Cha Mapinduzi (CCM), Japhet Hasunga, amesema akichaguliwa ataendelea kutoa huduma ya gari la kusafirisha miili ya marehemu wanaofariki dunia ndani ya jimbo lake ili kuwapunguzia gharama wafiwa.

Aidha Hasunga amesema akichaguliwa tena ataongeza gari la pili ili yawe mawili na yafanye kazi hiyo kwa ufanisi zaidi.

Amesema hayo Septemba 11 alipokuwa akiomba kura katika Kata ya Isalalo ambapo amewaomba wakazi wa kata hiyo wenye vitambulisho vya mpiga kura kuwapigia kura wagombea wote wa CCM siku ya Oktoba 29 mwaka huu.

Hasunga amewaomba wapiga kura wajiandae kumpigia kura mgombea wa urais kupitia CCM Samia Suluhu Hassan, mgombea Ubunge kupitia CCM, Japheti Hasunga na Mgombea Udiwani kupitia CCM kata ya Isalalo Happy Msokwa.

Kwa mujibu wa dereva wa gari linalosaidia kusafirisha miili ya marehemu Daud Mwambene wastani wa mwili mmoja umebebwa kila siku na kwamba siku nyingine alibeba miili hadi mitatu kwa siku.

Kuhusu ubebaji wa wagonjwa kutoka Zahanati au vituo vya afya kwenda hospitali kubwa amesema Serikali ya CCM imeleta magari matano kwenye jimbo lake ambayo yanafanya kazi kwenye vituo vya afya wakati wowote yanapoitwa.
Badala ya ku-improve huduma za afya huyu anazungumzia misiba, hivi huyu punda wa CCM anazo akili? Kwanini asitoe sasa, hadi achaguliwe. Huyu kweli mlevi.
 
  • Kicheko

Hiko ndo chama cha polepole mkuu🤣
 
Back
Top Bottom