Hata baada ya hili sakata la "hatuchezi tunacheza" tusitarajie jipya la maana labda kama hiyo bodi itatoka mbinguni

Hata baada ya hili sakata la "hatuchezi tunacheza" tusitarajie jipya la maana labda kama hiyo bodi itatoka mbinguni

FYATU

JF-Expert Member
Joined
Dec 7, 2011
Posts
5,882
Reaction score
5,087
Ukiwasikiliza hata wanaotoa maoni ya kushauri nini kifanyike utawasikia wakisema Yanga ni kubwa Simba ni kubwa.Hapa tayari ndio mzizi mkuu wa tatizo.

Kama Watu wana hofu kuwa Yanga wakipokwa pointi patachimbika ni nini litaleta utofauti huko siku za usoni iwapo moja ya timu hizi itafikia kupewa adhabu kama hiyo?.Leo hii Simba wanaamua kusema watacheza kwa kuwa tu huo ni msimamo tofauti na wa Wenzao,na ingeweza kuwa kinyume chake pia.Hao wanaodhani kwamba Yanga wasipocheza wakaadhibiwa patachimbika sasa ni lini kutakuja kuwa na bodi inayotoa maamuzi magumu dhidi ya timu hizi mbili?.

Mwisho wa siku tunazunguka mulemule tu kwa kufanya maamuzi ya busara,ambayo leo Yanga wanayaona hayafai kana kwamba wao hawajawahi kunufaika nayo,au basi sasa wapo tayari kwa maamuzi yatakayofuata sheria tu.Je hiyo ni kweli?.Kwa mtu mwenye akili timamu hiyo si kweli hata kidogo.

Kama bodi ya sasa haina uwezo wa kukata pointi au kuishusha daraja Simba au Yanga basi ni bodi ya Malaika gani tunaitarajia?.Hata siku ambayo Simba watagomea mechi na kutishiwa kushushwa daraja unafikiri hawatakuwa na sababu zinazoridhiwa na Mashabiki wao?je Mashabiki watakubali kushushwa daraja?.

Kikubwa ninachokiona mimi ni hizi timu kusaidiwa sana kuwa na Viongozi wenye busara na hekima nje ya hapo tutaendelea kukutana na mambo haya ya kitoto tu kila siku,mtaji wao ukiwa ni Mashabiki.

Na ni ajabu kwamba hata yule anayehofia vurugu iwapo Yanga wataadhibiwa wasipoingiza timu tena anakataa kwamba Simba nao wangefanya vurugu baada ya kuaminishwa na viongozi wao kuwa walizuiliwa kufanya mazoezi,kwamba Mashabiki wa Yanga wao ni raia wa kawaida na wale wa Simba ni Mawaiii na Makasisi wasioamini kwenye vurugu. Viongozi wenye hekima na busara.
 
Kipi bora ktk maisha kuanza vizuri ukamaliza vibaya?
Au kuanza vibaya ukamaliza vizuri?.
 
Kuanzia kufungwa kwa geti, kutishia kutokucheza kwa Simba, Mechi kughairishwa, kushtaki CAS ikijulikana wazi si kesi yenye hadhi ya kwenda huko, kupangiwa tarehe mpya ya kugomewa, kugomewa kwenyewe, yote unaweza kuta yanatokea sababu ya objective isiyohusiana na soka kabisa, objective ya kisiasa.
 
Back
Top Bottom