Bob Manson
JF-Expert Member
- May 16, 2021
- 4,158
- 7,787
Kumekuwa na wimbi kubwa la watu ambao hawaishi kuwasemea vibaya wahitimu wa elimu ya ngazi za juu hapa nchini. Ni kweli tatizo la ajira linazidi kuwa kubwa lakini sio sababu ya kulaumu na kuwasema vibaya wahitimu.
Huwa najiuliza, hao wanaokaa vijiweni na kuanza kuponda wanafunzi wa vyuo kwamba wanapoteza muda, Je majumbani mwao wana watoto? Kama jibu ni ndiyo, mbona wanapambana sana kusisitiza watoto wao waende shule na wasome kwa bidii. Kama wanaona elimu haina maana basi wasiwapeleke watoto wao shuleni.
huwa naumizwa sana na maneno ya watu (hasa ambao hawajasoma) kuhusu hili. Lengo la kusoma siyo kuajiriwa tu, sio lazma wote tuajiriwe wengine watafanya mambo mengine kwa kutumia elimu zao kama kujiajiri na kufanya ubunifu mwingine.