Hata kama leo hatujauzwa, ilitokea kesho tumeuzwa ni nani atajua?

Hata kama leo hatujauzwa, ilitokea kesho tumeuzwa ni nani atajua?

Logikos

JF-Expert Member
Joined
Feb 26, 2014
Posts
15,460
Reaction score
24,233
Kinachoendelea
Kuna maneno yanapita huku na kule yanachanganya..., wengine wanasema tumeuzwa wengine hatujauzwa; hata wale wanaobisha wengi wao hawana access ya information, zaidi ya hearsay za hapa na pale au fulani kasema na fulani hajasema au kilichoandikwa kinamaanisha hiki na sio kile.....

Hofu Yangu:
Iwapo haya mambo ni siri na hata hizi sintofahamu zimetokea kwa bahati mbaya baada ya haya makubaliano kuvuja (hivyo huenda tusingejua na lolote zuri au baya lingetokea bila sisi kujua mpaka pale ambapo matokeo hasi au chanya yametokea na kuishia kunyosheana vidole au watu kutolewa mbuzi wa kafara)

Au hata kama Makubaliano yakiwa mazuri leo ni kipi cha kuwakataza watu kuyabadilisha kesho na sababu ya Usiri kuweka vitu vya ajabu); Natoa Mifano Miwili:-

  • Iwapo TICTS walipewa Mkataba wa miaka 5 ili wachunguzwe wakifanya vyema iongezwe mpaka 10, lakini hata kabla 5 haijaisha ikaongezwa mpaka 15 (Je mwananchi wa kawaida alijua hayo)
  • Iwapo tuliambiwa (sio kuona) kwamba Mkataba wa Bagamoyo ulikuwa una madudu na hatujajua na mpaka kesho hatutajua sababu ya usiri, na kama hayo yanaweza kutokea ni kipi cha kumkata mtu ajaye kesho kuingia mkataba wa madudu zaidi ? Iwapo Rais mwenyewe alishangaa hayo madudu sisi wa mtaani kweli tuna uwezo wa kujua lolote ?
Suluhisho:
Sababu mwanadamu ni "Prone to Corruption" sio vema kumuachia au kuwaachia wachache ndio wakubaliane au waamue kwa manufaa ya nchi tena kwa USIRI. Kinga ni Moja Tu; Nayo ni UWAZI (TRANSPARENCY) Hii sio Mikataba / Makubaliano ya Ndugu wawili / marafiki wawili au Ukoo fulani ni Makubaliano kwa niaba ya wananchi wote na vizazi vijavyo.

Hivyo kama wanahisa wananchi hawa wanapaswa kujua mchakato mzima na mkataba mzima unasema nini mpaka nukta ya mwisho (USIRI NI KIFICHO CHA 10% na UPIGAJI) Kwanini tusubiri fulani atwambie badala ya wenyewe kuweza kusoma na Kama lugha ni ngumu kwanini iandikwe ngumu na isirahisishwe ili Bibi kizee wa kule Mpakani na yeye aweze kuelewa kinachoendelea kuhusu Mali yake.

Ni Ujuha kumuambia mwanahisa hii inamaanisha hivi na sio vile kwanini hayo unayomuelewesha yasiwekwe kwenye lugha ya mkataba na kueleweka ? Aliyesema format ya Mkataba / Makubaliano lazima yawe kama yalivyo ni Nani?

Bila uwazi tutaendelea kushangaa kila baada ya kuingia hasara, na hatutakoma tutaendelea na mikataba kama ya hivi mpaka pale chochote cha kuweza kufujwa kitakapofujwa, na hapo ndio tutabaki kunyosheana vidole kwamba sio fulani bali ni fulani ndio alifanya yaliyofanyika.
 
Ni kwa kuwa hatuna cha kuwafanya ndio maana tutaendelea kupigwa,tunge washikisha adabu hata siku moja wangekuwa wanaogopa kufanya upuuzi wao.
 
Wanaotuuza wameshaidiwa makazi huko wanapo panunua.

Siku niliposikia samia kaenda kwa mjomba wake omani. Na madalali wakapitia hapo hapo
 
Kama nilivyosema Baada ya Mshikemshike ya hapa na pale na Mikataba ishasainiwa we are non the Wiser....
 
Back
Top Bottom