Hata kama majigambo ni asili yao ila hii imezidi sasa, ni kabila gani hili wemeanza sifa za kuzika kwa kutumia crane?

Hata kama majigambo ni asili yao ila hii imezidi sasa, ni kabila gani hili wemeanza sifa za kuzika kwa kutumia crane?

NetMaster

JF-Expert Member
Joined
Sep 12, 2022
Posts
1,454
Reaction score
4,925
Ukisikia sifa zinaua ndio huku, Hapa kwa mporomoko huu wa jeneza sijui kama waliodondokewa na jeneza walipona?

Humo kwenye jeneza mwili wa marehemu ushavunjika vunjika kwajili ya hizi sifa.

Utasikia kisingizio ni jeuri ya pesa lakini ukifatilia unakuta pesa zenyewe ni mshahara wa kuajiriwa, hapo inabidi ushangae tu maana kuna makabila yana wafanyabiashara wakubwa ambao wanaingiza faida maradufu ya huo mshahara kila siku lakini kwenye misiba huwezi kuta hivi vitu.

Msiba ni maomboleza, huzuni, inafaa ichukuliwe hivyo na zaidi ni kuwafariji wahusika wa moja kwa moja, kuleta hizi mbwembwe na kusababisha taharuki kama hii ya kuanguka kwa jeneza ni kuzidi kuleta simanzi kwa wafiwa, kumkosea heshima marehemu, kuongeza gharama za msiba na hata kusababisha vifo vya ziada.

 
jeuri ya pesa qmmmmq
Muleba hapo, kijiji Kahumlo
Ni ushamba mtupu, mtu kipato chake ni cha kuajiriwa tayari anajiona pedeshee kisa anapokea mshahara, kuna makabila yenye wafanyabiashara wakubwa, faida tu ya siku ni mshahara wa mbunge lakini huwezi kuta haya mambo kwenye misiba yao.
 
[emoji3][emoji3][emoji3][emoji3] haki ya Mungu.
Ukisikiliza hayo amzungumzo sebo Gerald wafe, ni kiganda. Sebo ni Sir, gerald wafe ni gerald wetu.
So bila shaka hawa ni waganda
Ni kweli ni Waganda,sema Waganda na wa BK wote tabia zao zinafanana sana, nao ni watu wamajivuno Kama watani zetu wa BK!!
 
Ni kweli ni Waganda,sema Waganda na wa BK wote tabia zao zinafanana sana, nao ni watu wamajivuno Kama watani zetu wa BK!!
Hatari sana.
West afrika akifa mtu anahifadhiwa hata mwezi akiandaliwa mazishi sasa hizo mbwembwe za kwenye mazishi wahaya wakakae tena kwa kutulia kabisa.
Jamaa yangu mmoja muwest aliniambia sisi hatuwapendi ndugu zetu wakifa tunawahi kuzika kumalizana nao faster
 
Hapo mbio ilikuwa lazima, vipi km marehemu angeamka kwa mtikisiko ule!
 
Hapa kwa mporomoko huu wa jeneza sijui kama hakuna waombolezaji waliyofariki? Hii inatwa vifo juu ya kifo
 
😀😀😀😀 haki ya Mungu.
Ukisikiliza hayo amzungumzo sebo Gerald wafe, ni kiganda. Sebo ni Sir, gerald wafe ni gerald wetu.
So bila shaka hawa ni waganda
Kuna jamaa wako Kyaka nao wanaongea kama waganda
 
Back
Top Bottom