Nilichojifunza hapo ni kwamba Mh Tundu Lissu au chadema mna ungomvi binafsi na Mh JPM.
Hivi kukataa lockdown na huku nchi jirani zikiendeleza lockdown ni kaharibu mahusiano? Come ooon! Eti rafiki yake ni Burundi tu kwa sababu nchi ya Burundi huko nako walikataa lockdown!
Labda sijakuelewa mimi. Kama sijakuelewa ebu tutajie ni mahusiano gani kati ya Rwanda, Kenya, na Uganda Mh rais JPM ameharibu na kwa namna gani?
Mwanzoni ulisema eti Marafiki wa JPM ni kagame, Museveni na Hayati Nkurunziza leo umesema amaharibu mahusiano kati ya Kagame na Museveni.
Umesema eti JPM wakati wa Corona alienda kujificha chato. Chato siyo Tanzania? Au ni eneo la Burundi au Rwanda?
Kwani unajuaje Aliji-iisolate? Maana alituambia Mtoto wake aliugua Corona akajifukiza akapona? Kwani Corona inaogopa kumwambukiza mtu wa Chato?
Umesema eti amejenga uwanja wa Ndege wa chato. Kwani chato siyo Tanzania? Eti wanatumia Yeye na familia yake .hahahaaaaa.kweli usiyempenda utamnenea mabaya.Kwamba siku akifa atazikwa na uwanja huo wa chato na ndege pia, kwamba watoto wake siku moja watakuwa kuwa marais au matajiri na kununua ndege ambazo zitatumia uwanja huu tu.
Kipindi chote cha awamu ya tano,wapinzani hasa chadema na Tundu Lissu ugomvi wao ni Magufuli. Unaposema eti watanzania wameumizwa na utawala wa Magufuli siyo sawa hata kidogo.Ungesema badhi ya watanzania wameumizwa. Kama kweli wapo waliyoumizwa.
Watanzania wenye akili tungepafanya research kujua kwa undani kwanini Tundu Lissu na Chadema wana ugomvi binafsi maana siyo kwa Mtindo huu.