Nimekuwa nikitafakari dhana ya wazazi wetu waliyotumia kutoa majina yafuatayo kwa watoto wao nimekosa majibu. Mwana JF ambaye una weza kuwa na Ufahamu huo , naomba msaada. Majina hayo waliyo pewa watoto ni kama yafuatavyo.
1. Makaburi
2. Matatizo
3. Chausiku
4. Shida
5. Mapunda
6. Nguruwe
7. Kunguru
8. Sijali
9. Siwema
10. Sikitu
11. Sikuzani
12. Sikujua
13. Siyawezi
Wazazi wa zamani walipenda sana kuweka kumbukumbu ya matukia kwenye majina ya watoto wao, hivyo basi
1. Makaburi...... Inawezekana on the kwenda hospitari akazaliwa karibu na makaburi
2. Matatizo .......... Kulikuwa na ishu inawasumbua wazazi
3. Chausiku ..... Inawezekana usiku tu mama alikuwa anasumbuliwa na mimba ya huyu mtoto/ majina nya kizaramo
4. Shida ........... Alizaliwa kwa shida au kulikuwa na shida kali wakati anazaliwa
5. Mapunda ....... kuendeleza ungoni
6. Nguruwe kuendeleza ungoni
7. Kunguru ...... Inawezekana wakati anazaliwa kulikuwa na kunguru wengi sana
8. Sijali kizaramo zaidi aua wakati anazaliwa kulikuwa na tukio kwa wazazi hivyo hawakuwa wanalijali.
9. Siwema ... Pengine kuna watu wabaya waliwazunguka wakati wa ujauzito
10. Sikitu .... tukio limetokea wao hawakuona kama ni issue ya kujali
11. Sikuzani ... haikutegemewa either kuzaliwa salama au kutokea tukio fulani
12. Sikujua ... pengine ndo siku mzazi aliyopata kujuwa taarifa au jambo fulani
13. Siyawezi ... yaliyotokea hana nuwezo nayo