ukisema jina lina aksi maisha ya mjina siku za usoni hilo siyo sahihi sana maana maisha ya mtu au jamii huendana na msingi na mfumo wa maisha wanayoishi, rakini cha msingi zaidi mwenye kuamua maisha yawe namna gani ni mtu mwenyewe mhusika wa hayo maisha, wengi wamepatwa na misukosuko na matatizo katika maisha japo majina yao si akina shida, makoye, mawazo, sijari na kadhalika, kama jina linamchango katika mafanikio ya mtu kwanini akina Neema wote wasiwe na mafanikio tena yasiyo na mashiko? au akina Happy wasiwe na furaha milele?majina hasa ya kiafrika (nayaelewa) mara nyingi ni kumbukumbu ya tukio lililotokea kipindi ama ujauzito ulitungwa au kipindi mtoto anazaliwa kama ilivyo kwa akina Uhuru( kipindi nchi inapata uhuru) Nyerere( muda Nyerere anakuwa Rais Tanganyika) Kesi ( kuna kesi ilikuwa ikiendeshwa) nakaadhalika. upo hapo?