Hata kama ukinichukia.!

Mtambuzi

Platinum Member
Joined
Oct 29, 2008
Posts
8,809
Reaction score
15,421
Unapomchukia adui yako, haisaidii, sana sana unampa nguvu dhidi yako, dhidi ya usingizi wako, dhidi ya hamu yako ya kula, dhidi ya msukumo wako wa damu, dhidi ya afya yako, na dhidi ya furaha yako.

Adui yako anafurahi sana akibaini namna anavyokutesa na kukuumiza. Chuki yako dhidi yake haimuumizi kamwe, bali hugeuza maisha yako kuwa jehanamu ya kutosha.

Hii ina maana gani?

Ni kwamba, kamwe usimchukie mtu, kwani chuki hizo hazimuumizi huyo unayemchukia bali hukuumiza wewe mwenyewe. Ndio maana husemwa, Adui mpende tu!
 
Kuchukia ni part and parcell bana!
Maadui wengine bila kuchukiwa hawaelewi somo, atazidi kukukera!
 
Kuchukia ni part and parcell bana!
Maadui wengine bila kuchukiwa hawaelewi somo, atazidi kukukera!

Lakini uandhani anayeumia ni nani? sasa wewe mwenyewe ndiyo unajipa jakamoyo..............
 
Ni kwamba, kamwe usimchukie mtu, kwani chuki hizo hazimuumizi huyo unayemchukia bali hukuumiza wewe mwenyewe. Ndio maana husemwa, Adui mpende tu!

chochote unachomwombea mwenzio unajiombea mwenyewe.....................chochote unachomfanyia mwenzio wajifanyia mwenyewe.....................
"But I say to you, love your enemies, bless those who curse you, do good to those who hate you, and pray for those who spitefully use and persecute you........That you may be sons of your Father in heaven; for He makes His sun rise on the evil and on the good, and sends rain on the just and on the unjust." Mathew 5: 44-45.
 
maadui (kama sio maradhi na umaskini na ujinga) usipowachukia sasa ndo wanaweza kuelewa somo. ever heard of silence is the best answer? or sometimes u need to shut up in order to be heard? mtu anaefanya maudhi akikuona wakati wote una furaha anakuwa anajiuliza "what is she up to?". apostle paul aslisema 'nimepiga vita vilivyo VIZURI, mwendo nimeumaliza, imani nimeitunza'. its ok to choose ur battles, sio nzi unaua na bunduki, nyoka, na hata simba pia..
Kuchukia ni part and parcell bana!
Maadui wengine bila kuchukiwa hawaelewi somo, atazidi kukukera!
 
Ni ukweli usiopingika na wakati mwingine waeza mchukia mtu asiyeelewa hata kama unamchukia mwisho wa siku ni wewe mwenyewe unajiumiza na kujikosesha furaha na amani ya moyo wako the best way ni kusamehe ..........
 
Usimchukie lakini vilevile sio lazima um-entertain hata kumdharau tu kunatosha!!
 
nakuunga mkono; kumchukia ni kumpa ushindi; kwamba how much unaumia kutokana na alichokufanyia..............mpende ili asawajike ; kuwa pamoja na ubaya wote wewe umempenda na hapo ndio kwenye real punishment!
 
Usimchukue adui yako na wala usijikere nafsi yako vizuri akuone ukokama kawaida na muombe mungu amuweke aone mafanikio yako azidi kukereka...
 
Kumchukia mtu kweli haisaidii kumfanya aache kukutesa! Kumchukia mtu vile vile hakukupunguzii machungu bali kunayaongeza. Lakini chuki unaweza kuidhibiti, si kuizuia. Chuki ni response vile vile ambayo inaonekana inawasaidia watu kupambana au kulipiza kisasi.

Kuna utafiti ulifanyika marekani ikathibitisha kuwa kulipiza kisasi kunamsaidia mtendewa kupona kisaikolojia kuliko kitu kingine chochote (hili linahitaji mjadala mpana zaidi). Sasa chuki inapokuja inaonekana unakuwa unasukumwa na subconscious kuchukua hatua pale unapofanyiwa isivyo!

Mtu anapokufanyia vibaya, kumchukia huja "naturally" na haitokani na wewe kuamua. Pamoja na kuwa chuki inakusababishia mateso zaidi, lakini chuki ndo reality. Mara nyingi watu wanajifanya hawajachukia lakini deep inside wako moto. Chuki ni hisia, na kama hisia zingine inaweza kudhibitiwa si kuzuiwa!!
 

Kwa hiyo hao Wamarekani kwa kuwauwa Sadam Hussein na Muamar Ghadafi, ndio watakuwa wamepona kisaikolojia.......!? Kama huu utafiti ni wa kwao, basi watakuwa wanataka ku-justfy kile walichowafanyia maadui zao.......................
Kweli hili linahitaji mjadala mpana zaidi.
 
 
mi nachukia tu ajue hasijue na mtaani nalianzisha nikikutana nae
 
Kuchukia ni part and parcell bana!
Maadui wengine bila kuchukiwa hawaelewi somo, atazidi kukukera!
Ndiyo maana binadamu tukawa na nyongo, ukichekea kila kitu ni ishara ya khatari katika maisha. Hata mitume waliichukia dhambi na watenda dhambi sasa iwaje sisi tusichukie! Ukiniudhi mimi nakukata mabao, ukitaka geuza shavu la pili.
 
The best way to deal with your enemy ni kumpotezea wangu, akijua kuwa unampotezea na kumdharau, atajiona bonge la mjinga.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…