Mtambuzi
Platinum Member
- Oct 29, 2008
- 8,809
- 15,421
Unapomchukia adui yako, haisaidii, sana sana unampa nguvu dhidi yako, dhidi ya usingizi wako, dhidi ya hamu yako ya kula, dhidi ya msukumo wako wa damu, dhidi ya afya yako, na dhidi ya furaha yako.
Adui yako anafurahi sana akibaini namna anavyokutesa na kukuumiza. Chuki yako dhidi yake haimuumizi kamwe, bali hugeuza maisha yako kuwa jehanamu ya kutosha.
Hii ina maana gani?
Ni kwamba, kamwe usimchukie mtu, kwani chuki hizo hazimuumizi huyo unayemchukia bali hukuumiza wewe mwenyewe. Ndio maana husemwa, Adui mpende tu!