Hata kama unajua ni muhimu kujikumbushia nakuletea - basic driving test

Hata kama unajua ni muhimu kujikumbushia nakuletea - basic driving test

Afande Mwita sioni mwanafunzi wa kusomea driving kwa kudoji darasani akipita driving test hapa, bila nyekundu kadhaa imekula kwake 😂
 
Leseni zingetolewa kwa kujibu haya maswali nusu ya wamiliki wa leseni leo hii wangekuwa hawana leseni
Siku hizi lazima kuyajibu. Nimeona wakati ninaenda kurenew leseni yangu kule Oisterbay Dar es Salaam.

Sijajua mikoa mingine kama wanafanya hivyo

Ila wanaulizwa wale wanaoenda kuchukua leseni kwa mara ya kwanza.

Wanao-renew hutakiwa kwenda na cheti cha shule alichosomea
 
Mtihn wa udereva napiga 101 ata kama sijapitia driving school
 
Mwl mpwayungu anacomment wapi sasa. Usafiri wake yeye ni baiskeli
 
BASIC DRIVING TEST

1. Taja makundi ya alama za barabarani

2. Taja maeneo ambayo dereva haruhusiwi kuegesha gari

3. Chora mchoro wa alama ya onyo/Tahadhari ikionyesha watu wenye mtindio wa akili wapo eneo hili.

4. Taja matumizi ya taa za barabarani pia eleza kazi ya kila rangi ya taa za barabarani.

5. Taja ishara itakayo kutambulisha kwamba unao kuja mbele yako ni msafara wa kiongozi.

6. Taja maeneo manne ambayo dereva haruhusiwi kutipita gari la mbele yake

7. Ni muda gani dereva wa pikipiki anatakiwa kuwasha taa za pikipiki? na eleza kwanini?

8. Ukiwa kama dereva utafanya nini unapoona gari la wagonjwa linakuja mbele yako, likiomba kupewa kipaumbele

9. Toa maelekezo ni vipi utaendesha gari kwenye eneo lenye ukungu au vumbi?

10. Taja makundi nanne ya watumiaji wa barabara.

11. Nini kazi ya geji ya kilometa kwenye dashbodi ya gari?

12. Eleza kazi za
a) Taa ya ishara upande wa kushoto
b) Taa ya ishara unande wa kutia
c) Taa za ishara ziwakazo parnoja (double indicator)
d) Full tight (taa kubwa)
e) Deam light (taa kubwa)
f) Parking light

13. Ukiwa kama dereva unaelewa nini ukiona neno DOT 3

14. Eleza tofauti iliyopo kati ya D, D2 na L iliyopo katika gari la automatic.

15. Eleza sifa sita za dereva.

16. Taja geji sita zilizopo kwenye dashbodi ya gari.

17. Hatua gani utafuata pindi utapoteza leseni yako ya udereva.

18. Taja vifaa sita na nyaraka sita ambavyo dereva ni lazima awenavyo ndani ya gari akiwa safarini

19. Eleza umuhimu wa ukaguzi wa gari wa kila siku.4

20. Taja wajibu wa dereva akiwa anaendesha gari? 5

21. Taja kazi tatu za clach katika gari.

22. Taja kazí nne za engine oil katika gari.

23. Ukiwa kama dereva eleza kazí tatu za askari wa usalama barabarani.

24. Taja sehemu nne ambazo dereva haruhusiwi kupiga honi.

25. Taja hatua ambazo utafuata baada ya dereva kupata ajali?
1. Kundi la kwanza watu na la pili wanyama.
2. Hauruhusiwi kuegesha katikati ya barabara.
3. Siwezi kuchora kwa sababu hayupo alipelekwa Milembe.
4.Dah! Onasasa umeme umekatika.
5. Nitalirudia umeme ukirudi.
Samahani wameanza kuuza bia, nitaendekea baadae.
 
Back
Top Bottom