GE2025 Hata kama walikiuka kanuni Januari 19, 2025 bado Rais Samia ndiye bora kuliko wote wanaotamani kuwa wagombea wa CCM

Matukio, Taarifa, Habari na Mijadala ya Wananchi WAKATI wa Mchakato wa Uchaguzi Mkuu 2025
Sawa. Hao wengine wabaotaka kugombea ni akina nani...!!?
Wanaotaka kugombea ni kundi la Sukuma Gang likiwakilishwa na Polepole. Lakini wako pia akina Bashiru, Januari, Nape, Majaliwa, Luhaga Mpina to mention just a few
 
Yaliyofanyika wakati wa magufuli hayatoi uhalali wa kufanyika sasa. Swali jepesi ni kwamba kwa nini Rais hajawahi kukemea utekaji ulioshamiri sana nchi hii? Kwamba haoni? Hasikii? Wanaoteka wana pingu, bunduki na magari, wanayapata wapi? Uliwahi kumsikia IGP akikemea? Uliwahi kumsikia waziri wa mambo ya ndani akikemea?
 
Si atashinda hii October, tutaona kama kuna mradi mkubwa wa maana atakaoanzisha mpaka kufika 2030
mmoja wa miradi ambao umebuniwa ni Bonde la Msimbazi ambalo kutakuwa daraja na kingo za mto zitadhibitiwa kwa kujengwa kuanzia Kisarawe huko. Nyingine ni ya DMDP III ambayo inahusisha na majiji mengine kuboresha miundombinu ya barabara zake
 
Tunatiki
 
90% ya ulichoandika ni uongo mtupu
Zipinge takwimu zangu kwa takwimu na siyo kwa sentensi moja tu inayosema "ulichoandka hapo ni uwongo mtupu".

Maza kapiga kazi sana lakini Watanzania wanamchukia kwavitu 3; Uzanzibari, UIslamu na Uanamke basi
 
Kwa akili yako hayo kayafanya Samia?😂😂
 
Huu ni muda wa ccm kufanya internal regime change, sio muda wa kumpandisha mtu...
 
Ni bora kwako si kwa kila mtu.

Ya kiume yote hapo kakuta yapo in progress kumalizia yeyote anaweza hata mwehu!!

Shida nchi hii ni kuanza siyo kumalizia.
JK aliignia akaacha kumalizia barabara ya Nangurukuru _Kilwa ili kuiunganisha mikoa ya kusini kama ambavyo Mkapa alianzisha. Matokeo yake ni vurugu na uchomaji nyumba na mali za watu mwaka 2012 akati JK huyo huyo akitaka kujenga bomba la gesi kuja Dar.

Magufuli naye akatumia matusi yote kuuponda mradi wa Bagamoyo Port na akaacha kuendeleza Kinyerzi 4-5 ambazo zingetupa umeme wa gesi. Leo hii tungekuwa mabali sana kama Maufuli angekamilisha miradi ya JK.

Tumpe mauwa yake huyu Mama Samia kwa kuiendeleza na kuimaliza miradi iliyoanzishwa na mtamgulizi wake. Angeiacha ingekuwa hasara kwa Taifa maana ni kodi zetu
 
Its ok, tunajua wewe ni chawa mkuu lakini walau kidogo fanya analysis kwa kitumia walau akili ukiyopewa na muumba wako kidogo.
Kama ungekuwa na akili basi ungechagua angalao point moja ukaipinga kwa takwimu. Wewe ni mzembe fulani tu unaishi ka kutegemea ndugu wakati fursa zinapita
 
Uchawa kazi
 
Na mradi mwingine kausahau wa kuuza bandari za bara ambao Magu alikataa mpango huo
Fungua akili zako zitumie kwa mtazamo chanya. Achana na lugha ya kuuza bandari iliyotumika na wanaharakati bali angalia efficiency ya bandari iliyoletwa na DP world in terms of mizigo kuteremshwa, muda wa meli kusubiri kuingia na kutoka, kupanda kwa mapato nk
 
Anaelipinga hili anasumbuliwa na udini tu hakuna kengne, hakuna namna mama tunatamba nae
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…