Uchaguzi 2020 Hata Lissu mwenyewe sitaki atutawale miaka 10

Uchaguzi 2020 Hata Lissu mwenyewe sitaki atutawale miaka 10

ndege JOHN

JF-Expert Member
Joined
Aug 5, 2015
Posts
21,643
Reaction score
51,642
Mimi na familia yangu tumejadili sana kuhusu nafasi ya Urais na tumekubaliana kwamba lazima Magufuli apumzike ameshatutawala inatosha miaka mitano ni mingi sana na ukizingatia ameshakula maisha serikalini zaidi ya miaka 20.

Hatupo tayari atuongoze tena na sasa tutamchagua Lissu ila na yeye hatutampa miaka kumi akiwa Rais, miaka mitano inatosha kabisa kusafisha serikali kuondoa wale watendaji wabovu waliokaa ofisini na kutoka vitambi maofisa wavivu na wazembe.

Kiufupi huo ndo msimamo wetu, tunapiga maombi lolote litokee lakini sio kukubali kutawaliwa kwa miaka kumi na mtu yoyote.
 
Naiunga mkono familia yako,napenda hawa Wana siasa tuwe tuna wapiga tano nenda tano nenda ikizidi hapo wanatuzoea hawa!!

Sent from my Nokia C2 using JamiiForums mobile app

..na chama kinachotoa Raisi kisiwe na majority bungeni.

..hiyo itatuhakikishia participation ya vyama vyote ktk kuongoza.

..na tutakuwa tunafaidia mambo mazuri toka ilani za chama zaidi ya kimoja.
 
..asante sana.

..ungekuwa karibu yangu ningekununulia kinywaji unachopenda na nusu kuku na chipsi.

..Tz tunatakiwa tupate maraisi wa miaka mitano mitano kama watatu hivi ili wanasiasa waanze kuheshimu wapiga kura.
Hata wabunge pia ...hasa wa CCM wanapitisha sheria za kijinga kwa sababu wanajua tu watapita.
 
Mnaingiza Familia kwenye Majanga msio yajua.

Wewe ndege JOHN familia yako inakucheki tu. Wamama hawanaga mchezo na maamuzi yao. Subiri sanduku la Kura mkeo akampigie mtu mwingine.
 
Mkuu tukitaka kuendelea lazima tuhakikishe wanasiasa wanakuwa watumwa wetu siyo wao kuwa mabwana zetu kama ilivyo sasa,wanapaswa kututumikia na kutuogopa,ili iwe hivyo tunapaswa kuwa na utaratibu wa kuwapumzisha kila baada ya awamu ili wasituzoee na kufanya mambo kimazoea,
Mimi na familia yangu tumejadili sana kuhusu nafasi ya urais na tumekubaliana kwamba lazima Magufuli apumzike ameshatutawala inatosha miaka mitano ni mingi Sana na ukizingatia ameshakula maisha serikalini zaidi ya miaka 20...
 
Back
Top Bottom