Hata Magufuli angekuwepo angetakiwa kuchunguzwa kama DC Sabaya

OKW BOBAN SUNZU

Platinum Member
Joined
Aug 24, 2011
Posts
53,868
Reaction score
121,001
Kwa ufupi sana.

Tunaona mama akifanyia kazi malalamiko ya wananchi kuhusu viongozi mahalamia wanaotumia vyombo vya ulinzi kufanya unyanganyi na uporaji na ukandamizaji.

Kwa mambo ambayo alikuwa akifanya Magufuli dhidi ya wapinzani wake leo hii angekuwa hai alitakiwa kuondolewa kwenye urais na kuchunguzwa kwa kukiuka haki za binaadamu.

Usiniulize angechunguzwa na nani. Hoja yangu ni kwamba alikuwa na kila sifa za kuondolewa urais na kuchunguzwa kwa uvunjifu wa katiba ya nchi na haki za binadamu
 
Upuuzui mtupu kachunguze na wastaafu walio hai tuone kama walikuwa wema.
 

Kufa si kinga ya uchunguzi kutofanyika.

Naunga mkono hoja: uchunguzi ufanyike kuyaweka wazi kwa madhila yote ya awamu ya tano kama fundisho, ili mabaya yote yaliyotokea yasije kujirudia tena.
 
Upuuzui mtupu kachunguze na wastaafu walio hai tuone kama walikuwa wema.

Kushambuliwa kina Lissu, kupotea kina Ben, kupotea kina Azory, kuuwawa kina Mawazo, watu wa kwenye viroba nk, wewe unaona ni sawa tu mkuu?

Huoni haja kabisa kwa wahanga hawa na ndugu zao kutendewa haki?
 
Upuuzui mtupu kachunguze na wastaafu walio hai tuone kama walikuwa wema.
Hakuna kiongozi mwema, isipokuwa jiwe alikuwa na siasa za kishamba sana, toka tupate uhuru!!na ukatili wa waziwazi kabisa akijua hakuna wa kumfanya kitu, na ndio maana hao kina sabaya, makonda, walionekana mashujaa kwake!!yaani raia wako wanapotea tu, wanaopiga kelele juu yao unawaambia wakome, inawezekana hao ndugu zao wako nyumba ndogo!!wananchi wako wanakumbwa na baa la njaa unawaambia wafe tu serikali haina shamba!!MUNGU FUNDI
 
Kwa background ya sabaya akufaa kuwa mtumishi wa umma rekodi yake chafu sana
 
Kushambuliwa kina Lissu, kupotea kina Ben, kupotea kina Azory, kuuwawa kina Mawazo, watu wa kwenye viroba nk, wewe unaona ni sawa tu mkuu?

Huoni haja kabisa kwa wahanga hawa na ndugu zao kutendewa haki?
Wote lzm walipe damu hizi kama ulikuwa mlinzi ukafungua geti, ulikuwa dereva ukabeba mtu akauwawe ulitoa simu yako Ili wakauwawe hao jiandae, uzuri albadili ilishaponda nyoka kichwa waliobaki wote ni lzm wapukutike
 
Lipo wazi hilo kuna siku angechuchumalishwa kama Sabaya, amshukuru Mungu
 
Mama anapaswa kuunda tume
Wote waliofanyiwa unyama miaka mitano
Waende kuripoti .. kwenye ushahidi
Wahusika wapelekwe mahakamani ..
Na watu warudishiwe Mali zao walizo porwa
Bashite, musiba, wasiojulikana next episode ngoja sabaya apate uzoefu wa jela Kwanza awe nyapara
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…