Hata mswaki!

Hata mswaki!

Raia Fulani

JF-Expert Member
Joined
Mar 12, 2009
Posts
11,478
Reaction score
3,659
Kiswahili kweli si chetu. Chetu ni lugha mama. Nimeona kwenye cnn mwarabu akimwonyesha ripota. And this is "miswaki". Ya vijiti lakini. hata hili neno kumbe tumedesa!
 
haha, habari ndyo hiyo...
 
Kiswahili ni lugha ambayo asili yake inatokana na biashara iliyoanzia pwani ya Afrika Mashariki. Wafanyabiashara kutoka nchi mbalimbali wkijumuika na wenyeji walivumbua lugha ambayo walikuwa wanaelewana katika biashara na mawasiliano. Hiyo usishangae kuwa katika Kiswahili kuna kiarabu, kibantu, kiingereza, kijerumani, kireno, kihindi, kichina n.k. Kwa ufupi Kiswahili ni lugha yetu haswa!
 
Nakubaliana nawe kabisa mkuu. Na isitoshe lugha hukua kwa njia mbalimbali mojawapo ikiwa ni kuazima 'to borrow' misamiati kutaka lugha nyingine.
 
sijasema kama kiswahili ni chetu ila sisi tujivunie lugha zetu za asili tu. Kiswahili kimetohoa mno! Ni sawa na mtunzi wa kitabu aliyejaza references kibao. Hana cha kujivunia kwani katumia zaidi mawazo ya watu wengine
 
Kiswahili kweli si chetu. Chetu ni lugha mama. Nimeona kwenye cnn mwarabu akimwonyesha ripota. And this is "miswaki". Ya vijiti lakini. hata hili neno kumbe tumedesa!

Hata ilo neno Sawahil (swahili) pia tumekopa.

Jina la 'Kiswahili' linatokana na wingi wa neno la Kiarabu sawāḥil (سواح&#1604😉 nalo ni sāḥil (ساح&#1604😉, maana yake "Mpaka (boundary)" au "pwani" (hutumika kama kivumishi kumaanisha "watu wa pwani" au, kwa kuongeza neno 'ki-' ina maanisha "pwani ya Waswahili").

Neno Lugha, Lakini yote yana asili ya Kiarabu...!
 
Kiswahili kweli si chetu. .. And this is "miswaki". Ya vijiti lakini. hata hili neno kumbe tumedesa!

Labda hatukuwa na miswaki (tulikuwa hatupigi mswaki), kama ambavyo hatukuwa na meza (kireno), shule (kijerumani) n.k., n.k.
 
Hata ilo neno Sawahil (swahili) pia tumekopa.

Jina la 'Kiswahili' linatokana na wingi wa neno la Kiarabu sawāḥil (سواح&#1604😉 nalo ni sāḥil (ساح&#1604😉, maana yake "Mpaka (boundary)" au "pwani" (hutumika kama kivumishi kumaanisha "watu wa pwani" au, kwa kuongeza neno 'ki-' ina maanisha "pwani ya Waswahili").

Neno Lugha, Lakini yote yana asili ya Kiarabu...!

mkuu kwa 'staili' hii kazi tunayo
 
Labda hatukuwa na miswaki (tulikuwa hatupigi mswaki), kama ambavyo hatukuwa na meza (kireno), shule (kijerumani) n.k., n.k.

kifupi tukubali kuwa ustaarabu tumefundishwa na wageni
 
Mziwanda, unategemea nini lugha ambayo imechukuwa almost 40% ya misamiati kutoka Lugha nyingine?

Kwenye sentesi moja tu ya kiswahili sidhani kama unaweza kukosa neno la kiarabu...! Ni ngumu sana kwa sasa kupata lugha ambayo haina mkopo kutoka lugha nyingine...!
 
ni kweli ila kwa kiswahili ni too much. Labda lugha nyingine iliyokopa sana ni kifaransa, toka kingereza
 
Kiswahili kweli si chetu. Chetu ni lugha mama. Nimeona kwenye cnn mwarabu akimwonyesha ripota. And this is "miswaki". Ya vijiti lakini. hata hili neno kumbe tumedesa!

Swahili = Bantu + Arabic
 
[B said:
Kekuye[/B];688031]Nakubaliana nawe kabisa mkuu. Na isitoshe lugha hukua kwa njia mbalimbali mojawapo ikiwa ni kuazima 'to borrow' misamiati kutaka lugha nyingine.

Unajina zuri ile mbaya
 
unashangaa mswaki, wakati hata neno samaki tumepiga desa.
Hata neno Kanisa pia... Neno Rais... Jamhuri, Waziri, wizara, Almashauri, Serikali, Kitabu, Makataba, Dunia, Binamu, Binti.... Na hata jinsi ya kuhesabu.
 
Kumbe ndo maana hata 'chaguo la mungu' anaruka kila mara kwenda kudesa nje! Juzi kaenda kudesa kubembeaaaa duh!
 
Back
Top Bottom