Hata nikitumika miaka kumi, Siwezi kuondoka Yanga kwasababu ya kukosekana hela

Chukwu emeka

JF-Expert Member
Joined
Jan 12, 2018
Posts
24,314
Reaction score
38,919
Habari wanaJF,ni imani yangu mnaendelea vema na kazi.

Leo katika kipindi cha Kipenga Extra kinachoruka kuvitoa East Africa Radio kuanzia saa 6 mchana hadi saa 7,aliarikwa,head coach mkuu wa Yanga,Papa Mwinyi Zahera katika kipindi ambacho host wake ni Goza Chuma.

Alipoulizwa iwapo ataondoka kwasababu ya kutolipwa,akajibu Siwezi kuondoka Yanga kwasababu ya kutolipwa Maana najua sikumoja nitalipwa cos nina mkataba nao,hata nikikaa miaka kumi najua nilalipwa hata kwakwenda fifa.Alipoulizwa ameijuaje Yanga akasema ameijua kupitia mdogo wake ambaye ni mfanyabiashara mkubwa nchini Kenya na huyo mdogo wake ni rafiki mkubwa wa ndama ambaye ni moja ya wanachama waandamizi wa timu yetu ya wananchi.

Akijibu swali la anawaonaje wachezaji wa Tz alisema wengi wanakosa physical exercise, hivyo aliamua kutoa hela yake mfukoni kununua vifaa vya kusoma work rate ya wachezaji wanapokuwa mazoezi,hivyo kuifanya Yanga kuwa fit na wachezaji kutochoka kwa dakika zote 90.Na Mwinyi anaonyesha kuwa anaishi na wachezaji wake kama familia moja.

Yanga tukiwekeza vema huyu Kocha tukampa muda anaweza kutuvusha na kutufikisha mbali sana.

Daima mbele,Nyuma mwiko💪💪💪💪💪
 
Ujanja ujanja wa kibongo ndio utakaomfukuza huyu kocha,japo yeye ana mapenzi ya moyoni kabisa na Yangu. Ana falsafa za kizungu,ukweli wa wazi kwenye ukweli,hana kupindisha pindisha kama walivyo wabongo

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Huyu jamaa anafanya mpira as a passion.....!
Vile katukuta katika nyakati mbaya na katika nyakati hizo anaonyesha ubora wake......!

Sent using Jamii Forums mobile app
Nyota ya jamaaa ipo fresh sema ni kuiombea sana hii timu. Hali sio nzuri.

Ila hamasa ya kocha tuu ndio inafanya isonge mbele. Siku wakianza kupoteza game hata moja itawaathiri saana

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Hii ni habari njema kwa Yanga na familia ya wanayanga, ila ukiiangalia kwa jicho la tatu inaonesha jinsi gani soka letu lina matatizo makubwa sana, hizi timu kubwa Tanzania zina miaka zaidi ya themanini lakini inafikia hatua zinaendeshwa kwa kuungaunga namna hii ni hatari.
Kama tutaenda mwendo huu kushindana kimataifa itakuwa ndoto tu. Hatuwezi shindana na timu zinazoendeshwa kiuweledi ktk hali ya namna hii.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Upo sahihi kabisa mkuu, sasajiulize Timu kama ndanda watakuwaje kama Yanga tunahangaika ivi
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…