Nashukuru mkuu, baada ya kunipatia uzito na urefu wako, nilibaini kuwa pamoja na kuwa unakula mara kwa mara lakini bado hakukuwa na madhara hasi sana kwa kuwa ungekuwa unakula kula mara kwa mara na uzito wako unazidi kiasi unachopaswa kuwa nacho, basi hilo ndilo lingekuwa tatizo zaidi.
Kwa kawaida kila mtu ana mazoezi yake yanayomfaa kufanya ambayo yanaendana na mwili alio nao, wengi wetu hatufuatilii jambo hili, ukiwaza kuinua vyuma, unainua, ukiwaza kukimbia, unakimbia. Mazoezi yeyote tu bila kujiuliza iwapo mwili unahitaji mazoezi ya aina hiyo.
Aina ya mazoezi unayofanya yanawafaa watu wenye uzito uliozidi (overweight/obesity), wewe inakutosha tu kutembea kwa miguu kwa mwendo wa haraka kidogo lisaa 1 mara 5 kwa wiki. Metabolic rate yako itapungua na njaa itashuka.
Jitahidi kunywa maji glasi 2 (ml 500) kila nusu saa kabla ya kula, maji ya kawaida siyo ya kwenye friji. Unaweza pia kuongeza uzito wako hata kilo 6 zaidi kama utataka.
Jisomee kurasa 2 zifuatazo:
http://maajabuyamaji.net/maajabu/uzito-kupita-kiasi/ na
http://maajabuyamaji.net/new-page/jitibu-kwa-kutumia-maji/