Jamaa mmoja alikuwa ni mlevi wa kupindukia wa pombe za kienyeji,ikafika wakati akaamua kuacha kunywa pombe na kuithibishia jamii kwamba yeye na pombe basi tena.
Siku moja baada ya muda mrefu kuacha ulevi, alikutwa bara anakunywa bia.Kwa mshangao jamaa wakamuuliza "wewe si ulisema umeshaacha kulewa,mbona unakunywa bia?
"Yule mlevi akawajibu mbona Pele amejiuzulu kucheza mpira lakini anapiga danadana?