Hata Rais hudanganywa: Njama za Ikulu ndizo hizi

Robert Heriel Mtibeli

JF-Expert Member
Joined
Mar 24, 2018
Posts
28,297
Reaction score
68,017
HATA RAIS HUDANGANYWA; NJAMA ZA IKULU.

Na, Robert Heriel

Soma mpaka utakapoamua kuishia, masuala ya kuambiana andiko refu hayo achana nayo, nimeandika refu kwa sababu wapo wanaopenda maandiko marefu, wewe unayependa andiko fupi soma utakapoishia.

IKULU ni maskani yaliyorasmi anayoishi Rais na kufanyia shughuli zake. Ni moja ya sehemu nyeti katika taifa lolote kwani kiongozi wa nchi huishi humo.

Hakuna Rais au Mfalme Duniani ambaye hajawahi kudanganywa alipokuwa kwenye utawala. Marais na Wafalme wote wameshawahi kudanganywa ingawa inawezakana uongo huo ukatofautiana.

Marais Wastaafu kuanzia Hayati Baba wa Taifa, Mwl Julius Nyerere, na Hayati Benjamini Mkapa, Rais wa amamu ya tatu, kisha waliohai ambao Ni Mzee Mwinyi, Mzee Kikwete, na sasa tuna Mhe, Rais, Dkt John Pombe Magufuli. Wote kwa namna Moja ama nyingine wataungana na mimi kuwa kuna wakati walidanganywa. Narudia hakuna Kiongozi ambaye hajawahi kuingizwa mjini na ndevu.

Rais anapoingia tuu madarakani kabla hajafanya jambo lolote, kitu cha kwanza ni kuteua watu watakaomzunguka na kushirikiana naye katika utawala wake. Hili ndilo jambo la kwanza kabisa na muhimu kwa mtawala yeyote anapoingia utawalani. Na hapa ndipo mwanzo wa kufaulu au kufeli.

Rais au Mfalme anapoteua watu hao watakaomtumikia anakuwa anazingatia sifa zifuatazo;
1. HEKIMA, AKILI na MAARIFA
2. ASILI YA UONGOZI NA MASHUHURI
3. ELIMU
4. WAZURI WA UMBO NA SURA
5. NIDHAMU NA ADABU

Mambo hayo matano ndiyo huongoza Rais na wafalme kuteua timu itatayomsaidia katika utawala. Kila sifa inamaana yake na ni nyeti kwa kazi maalumu za kiutawala. Wafalme na viongozi wengi walioenda kinyume na sifa tajwa hapo juu waliingia hasara, waliumia, na mara nyingi falme zao zilidondoshwa mapema sana.

Rais iwe kwa kujua au kutokujua ni lazima ajikute anateua watu wenye sifa hizo ili asije akapata hasara katika utawala wake, kupata hasara ni kushindwa kuongoza watu na mwishowe kulalamikiwa kila mara ingawaje lawama haziishi kwa mwanadamu lakini walau ziwe lawama chache.

Nianze mada hii kwa kunukuu kitabu cha Daniel 1
Danieli 1:
3. Mfalme Nebukadneza akamwamuru Ashpenazi, towashi wake mkuu, amchagulie baadhi ya vijana wa Israeli wa jamaa ya kifalme na ya watu mashuhuri.
4. Mfalme alitaka vijana wasio na kasoro, wazuri kwa umbo, wenye uzoefu wa kila hekima, wenye akili na maarifa na wanaofaa kutoa huduma katika ikulu. Alitaka pia vijana hao wafundishwe kusoma na kuandika lugha ya Wakaldayo.

Huyo ni Mfalme Nebukadneza akihitaji timu mpya ya vijana watakaomtumikia ambao walitekwa huko Yuda na kuletwa Babiloni.

Rais lazima azungukwe na watu wenye akili, werevu, wenye hekima, ujuzi na maarifa ya kila namna, wazuri wa maumbo na sura, na wenye nidhamu na adabu.
Thadei Ole Mushi Aliwahi andika katika makala zake kuwa Watu wenye akili ni mali ya Rais. Nami namkubali kwa asilimia mia moja. Kwa sababu naelewa maana ya statement hiyo.

Ikulu kuna njama, hila, ulaghai na kuingizwa mkenge kienyeji na kisasa. Ni lazima Rais awe na watu wenye akili za manufaa karibu kwa kila kitu anachotaka kukifanya hasa vile vitu vinavyogusa maisha ya watu moja kwa moja.

Baada ya Uteuzi wa watakaomtumikia Rais au Mfalme kinachofuata ni kutolewa kwa elimu kwa hao walioteuliwa kabla hawajaingia mzigoni yaani kufanya kazi. Inafahamika kuwa hata kama mtu anahekima au akili za namna gani hawezi kujua mambo yote hivyo ni muhimu kum-brush kidogo ili aendane na mazingira ya kazi.

Baada ya elimu kutolewa kinachofuata ni kwenda kazini. Hapa ndipo shughuli ilipo kwani kila mtu anataka kufanya kazi zaidi na zaidi ili Rais au Mfalme amuone kuwa ni mfanyakazi bora. Kikawaida huwa nawaambiaga watu kipindi cha awali sio kipindi cha kumfanyia mtu assessment kwani mara nyingi kipindi hicho watu ndio hujifanya wachapakazi ili kumpendeza kiongozi wao(Rais) na kujenga uaminifu.

Kikawaida yule anayeanzaga vizuri kwa mbwembwe ili kuichota akili ya Boss ndiye baadaye huwa mbaya, na yule ambaye hufanya kazi kawaida huja kuwa mtumishi mzuri. Bahati mbaya ni kuwa wale vihere here mwanzoni mara nyingi ndio hupewa zaidi nafasi nyeti na wale wanaofanya kazi kawaida huweza kufukuzwa mpaka kazi.

Siku zote wale wanaotaka kuonekana mbele ya Rais au Mfalme ndio mara nyingi huunda njama, hila, na ulaghai kwa Rais au Mfalme. Ni rahisi kwa watu hao kufanya hivyo kwa sababu tayari wamejenga uaminifu kwa Rais au Mfalme. Hata mapinduzi karibu yote duniani yamefanywa na watu walioaminiwa na wafalme na Rais, yaani waliokaribu na Rais.

Kiutawala, mtu yeyote anayetafuta kwa kila namna kukufanya umuamini ni mtu hatari na kuwa macho naye, kwani wengi ndio huwa na matatizo ndani ua utawala wako. Rais waliongoza nchi hii watanikubali kuwa mambo makubwa waliokwama basi nyuma ya mambo hayo alikuwepo mtu aliyemuamini na aliyempa nafasi kubwa.

Sasa turudi kwenye mada;

Wateule wa Rais huanza kuoneana wivu na kijicho kutokana na kuwa kwa kadiri muda uendavyo lazima Rais awe na wateule anaowapenda zaidi kuliko wengine. Hapa ndio kizaazaa huanza, kwani hakuna asiyetaka kupendwa na Rais au Mfalme labda wale wenye Itikadi za kimungu, wazee wa haki.

Kisa cha Daniel ni kisa cha kisiasa katika mambo ya utawala kwani maisha yake yote ya ujana mpaka uzee ameishi akitumikia Ikulu. Hivyo kama kuna mtumishi yupo Ikulu au sehemu nyeti basi kama kuna mtu anapaswa amfuatilia zaidi ndani ya Biblia basi ni Danieli.

Baada ya wenye hekima, wachawi na vigagula, waganga na wasihiri, wakaldayo kushindwa kutafsiri ndoto ya Mfalme Nebukadneza, Mfalme alighadhibika hata akafikia hatua akataka kuwaua, Kumbuka watu hawa ni wateuliwa wa Mfalme kwa kazi za namna hizo, sasa kama mfalme anakulipa kwa kazi hizo alafu unashindwa kutafsiri ndoto kazi kula mshahara wa bure, hulipi kodi, mfalme akaona hawa kumbe wananiibiaga, akataka kuwaua.

Lakini Daniel akawaokoa baada ya kusikia habari hizo, akamwambia mfalme asiwaue bali yeye apewe siku tatu na kama naye atashindwa kutafsiri ndoto hiyo basi yeye na hao waganga, wachawi na vigagula wauawe kwa kukatwa kichwa. Mfalme akasema hewala.

Kweli Daniel, akafaulu kutafsiri ndoto. Mfalme akafurahi akampa heshima kubwa na kuzidi kumpa cheo ndani ya Babeli, Daniel akaona awape promo rafiki zake wa tatu ili mfalme nao awape kazi. Mfalme akakubali, na wateuliwa wapya wakateuliwa ambao ni Shadrack, Meshack, na Abednego.

Kumbuka kwa jisni Daniel anavyopanda cheo basi jua kuna wanaoshushwa, kumbuka kuingizwa na kuteuliwa kwa kina Meshack ni kushushwa kwa wengine. Unafikiri walioshushwa watafurahi? Ni kwamba maslahi yao yatashuka, heshima yao itashuka kama sio kuondoka kabisa. Sasa wapo tayari kwa jambo hilo?

Unafikiri wazee wa kikaldayo na wababeli watachekelea kuona vijana wa kiyahudi ambao muda huo ni mateka nchini Ashuru kwenye mji wa Babeli wataona raha. Jibu ni hapana.

Hapo ndipo njama, hila, fitina na kila aina ya ulaghai utafanyika. Hapo lazima mfalme awe makini kwa maana hao hao aliowateua ndio watamuangusha kama asipokuwa makini.

Basi wazee wa hekima kuona Daniel anaongeza wenzake, na wamepewa cheo, wakaunda njama yenye akili.
Wakamshauri Mfalme atengeneze sanamu kubwa lile lile aliloliota na Daniel akamtafsiria. Kisha litakapotengenezwa liwe la dhahabu mwili mzima kuashiria ufalme wa Nebukadreza utadumu milele, alafu watu wote waje kulisujudia na kuliabudu. Hhahahah! Unaona njama hiyo. Hapo lazima Mfalme bila kujua lazima aingie kingi. Na kweli akajenga hilo Sanamu kubwa la Dhahabu, kisha mbiu ikapigwa watu waje kulisujudu kama ilivyoamriwa na Mfalme.

Kumbuka vijana wa Daniel wale watatu ni Wayahudi na dini zao haziwaruhusu kusujudia Sanamu. Sasa Amri hii lazima iwachonganishe na Mfalme.

Watu walipokuja kusujudu, wale vijana watatu wakakakataa, wale wazee wakaenda kushtaki kuwa kuna vijana watatu wale mateka uliowateua mfalme wamekataa kuitii amir yako. Hapo hapo Mfalme akajua ilikuwa ni njama ya wale wazee, akajua ilikuwa hila ya wale wazee kuwaangusha vijana wale baada ya kupewa cheo. Lakini mfalme hakuwa na jinsi alishaingizwa mkenge na wahuni na akasaini sheria isemayo watakao kataa watatupwa kwenye tanuru la moto.

Lakini Mfalme kwa vile anajua hila hizo, akajaribu kuwatetea vijana hao watatu, akawaita kisha akawauliza kupata uthibitisho wa madai yale, vijana wakasema ni kweli. Mfalme akahamaki kwa ghadabu lakini bado akataka kuwatetea akawaambia, itapigwa baragumu kwa mara ya pili, alafu mkiisikia wote mtasujudia ile sanamu ya dhahabu ya mfalme, kama ilivyo amri ya mfalme. Vijana wakamwambia hauna haja ya kupiga mbiu tena kwani sisi hatutaisujudia sanamu yako. Ni heri kumtii Mungu kuliko mwanadamu. Mfalme hakuwa na jinsi ilibidi aamuru watupwe kwenye tanuru la moto. Walitupwa lakini Mungu akawaepusha.

Huo ni mfano wa njama au hila zinazofanyika katika majumba ya wafalme au Rais.

Mfano wa Pili; Daniel 6;
Daniel 6;
1. Mfalme Dario aliamua kuteua wakuu 120 kusimamia mambo ya utawala.
2. Aliwateua pia wakuu watatu, Danieli akiwa mmojawapo, wawasimamie wale wakuu wengine na maslahi ya mfalme, asije akapata hasara.
3. Muda si muda, Danieli akadhihirika kuwa bora kuliko wale wasimamizi wengine na wakuu wote kwa kuwa alikuwa na roho njema. Hivyo mfalme akanuia kumpa uongozi wa ufalme wote.
4. Wale wakuu pamoja na maliwali wakatafuta kisingizio cha kumshtaki Danieli kuhusu mambo ya ufalme, lakini hawakuweza kupata sababu ya kumlaumu, wala kosa lolote, kwani Danieli alikuwa mwaminifu. Hakupatikana na kosa, wala hatia yoyote.
5. Ndipo wakapatana hivi: “Hatutapata kisingizio chochote cha kumshtaki Danieli isipokuwa kama kisingizio hicho kitakuwa kinahusu sheria ya Mungu wake.”

Hahaha! Mambo ya teuzi hayo. Kabla hujang'ang'ania teuzi jiulize unaziweza njama, je una-balen dio ya Fitina na hila. Kama huna ni bora utulie zako tuu. Au je unajua kusimamia haki? kama hujui jiachie zako tuu, njoo kwa Taikon akupe shamba ulime karanga.

Daniel amedumu Ikulu kwa awamu tatu za utawala. Utawala wa Mfalme Nebukadneza, Mfalme Belshaza(mtoto wa Mfalme Nebu) huyu alipenda kumuita Daniel Belteshaza ambalo ni jina la Mungu wake(mungu wa Belshaza) na mwisho alikuwa Mfalme Dario kutoka umedi yaani taifa wa wamedi.

Hii ni kusema Daniel sasa anauzoefu kwenye majumba ya kifalme, hivyo tunategemea anaouwezo wa kukabiliana na Fitina, hila na njama.

Wateuliwa ndio huweza kumfanya Rais afanye kazi vizuri au ahahribu. Hawa ndio humshauri Rais kwa zaidi ya 90%. Hizo 10% ndio huamuliwa na Rais au Mfalme. Marais wote watakubaliana na mimi hivyo. Ukiona Rais ni dikteta basi jua timu yake kwa kiasi kikubwa ni madikteta na wameamua iwe hivyo.

Sasa Daniel kafanya vyema, kapata ujiko kwa Mfalme, wenzake badala wampongeze wanamuundia zengwe, hahahah!.

Kumbuka watu karibu wote wanaomzunguka Mfalme au Rais wanaakili sasa inategemea wanazitumia kwa njia njema au mbaya. Hivyo kuunda zengwe au njama bila Rais au Mfalme kujua ni jambo rahisi kwao kwa sababu nilishasema wanaakili na maarifa ya kila namna.

Wakatathmini namna ya kumuangusha Daniel, wakaja na jibu kuwa, Daniel sheria za Mungu wake ndio kete yao muhimu.
Wakaenda kwa mfalme Dario wakamwambia, naomba ninukuu hapo chini;
Daniel 6;
6. Basi, hao wakuu na maliwali kwa pamoja, wakamwendea mfalme na kumwambia, “Uishi ee mfalme Dario!
7. Sisi wakuu uliotuweka, wasimamizi, maliwali, washauri na wakuu wa mikoa, sote tumepatana kuwa inafaa, ee mfalme, utoe amri na kuhakikisha inafuatwa kikamilifu. Amuru kwamba kwa muda wa siku thelathini kusiwe na mtu yeyote atakayeruhusiwa kuomba kitu chochote kwa mungu yeyote au kwa mtu yeyote, isipokuwa kutoka kwako wewe, ewe mfalme. Mtu yeyote atakayevunja sheria hii na atupwe katika pango la simba.
8. Hivyo, ee mfalme Dario, utoe amri hiyo na kuitia hati sahihi yako ili isibadilishwe. Nayo itakuwa sheria ya Wamedi na Wapersi, sheria ambayo haibatilishwi.”
9. Hivyo, mfalme Dario akaitia sahihi hati ya sheria hiyo

Unaona mambo hayo! Hiyo inaitwa Rais au Mfalme kuingizwa Mkenge. Kumbuka Mfalme hapo hana hili wala lile, kwanza wamemsifia, pili wametaka mungu wake yaani mungu wa Dario ndio aabudiwe pekeake kwa hizo siku thelasini yaani mwezi mmoja.
Hapo walijua kuwa Daniel hawezi kuabudu mungu mwingine isipokuwa Mungu wake, pili hata asipoabudu pia, hawezi kukaa siku thelasini bila kumuomba Mungu wake, kumbuka Daniel kwa siku huomba mara tatu majira ya mchana. Unaona njama hiyo.

Mwisho ili kummaliza kabisa Mfalme wakamwambia iwe sheria na aweke saini yeye mwenyewe ili watu wasijeleta ukorofi. Kumbe nia yao sio watu bali ni kumtia kitanzi Mfalme mwenyewe kuwa kama atagundua hila yao basi asiwe na uwezo wa kutengua maamuzi yake. Hahahah! Mfalme kaingia kingi bila kujua. Kazi kwishaa!

Daniel hizo habari akazipata lakini hazikumtisha, kweli akakaidi amri kama walivyotarajia wateuliwa wenzake. Dili likawa linaenda sawasawa na lilivyopangwa. Mfalme anapewa taarifa kuwa Daniel amekataa kufuata amri yake ndio akagundua kuwa jambo lile halikuwa na nia ya kumfurahia yeye kama Mfalme bali kumuangamiza Daniel. Alisikitika sana.
Naomba ninukuu ili twende sawa;
Daniel 6;
11. Watu wale waliofanya mpango dhidi ya Danieli waliingia ndani, wakamkuta Danieli akiomba dua na kumsihi Mungu wake.
12. Basi, walikwenda kwa mfalme na kumshtaki Danieli kwa kutumia ile sheria, wakisema, “Mfalme Dario, je, hukutia sahihi hati ya sheria kuwa kwa muda wa siku thelathini hakuna mtu yeyote atakayeruhusiwa kuomba kitu chochote, kwa mungu yeyote, au kwa mtu yeyote isipokuwa kutoka kwako wewe, ee mfalme, na kwamba yeyote atakayevunja sheria hii atatumbukizwa katika pango la simba?” Mfalme akaitikia, “Hivyo ndivyo ilivyo, kulingana na sheria ya Wamedi na Wapersi ambayo haiwezi kubatilishwa.”
13. Wakamwambia mfalme, “Yule Danieli aliye mmoja wa mateka kutoka nchi ya Yuda hakuheshimu wewe mfalme wala haitii amri uliyotia sahihi. Yeye anasali mara tatu kila siku.”

Unaona! Unaona! Hahahaah! Mfalme kaingia kwenye kumi na nane za wahuni aliowateua kazi yake ni kusema ndio tuu, na ukizingatia ni lazima aseme ndio kwani ni kweli alikubali na sheria za wamedi hazibadiliki.

Tumalize mchezo hapa, Mfalme akiwa keshaenda Kibla.
Daniel 6;
14. Mfalme aliposikia maneno hayo, alisikitika sana. Akajitahidi sana kupata njia ya kumwokoa Danieli. Aliendelea kujaribu mpaka jua likatua.
15. Wale watu wakamwendea mfalme Dario kwa pamoja na kumwambia, “Ee mfalme, ujue kuwa hakuna sheria wala amri yoyote ya Wamedi na Wapersi inayoweza kubatilishwa baada ya kuwekwa na mfalme.”

Masikini Mfalme Dario keshajua ameingizwa mkenge. Katapeliwa na wajanja.
Mwishowe Daniel alitupwa kwenye Tundu la simba kwa sababu hakukuwa na jinsi kwani wajanja walidizaini mchongo kiasi kwamba hawakutoa nafasi ya Daniel kuokoka.
Baadaye Daniel aliokolewa na malaika kwa kutoliwa na simba. na haya ndio maneno ya Mfalme Dario alipodamka alfajiri kwenda kuona kama Daniel ameliwa na simba au yu ngali hai, kwani usiku mzima moyo wake ulifadhaika sana.

Daniel 6
18. Kisha mfalme akarudi katika ikuluni yake ambamo alikesha akifunga; hakufanya tafrija ya aina yoyote, na usingizi ukampaa.
19. Alfajiri na mapema, mfalme Dario aliamka, akaenda kwa haraka kwenye pango la simba.
20. Alipofika karibu akamwita Danieli kwa sauti ya huzuni, “Danieli, mtumishi wa Mungu aliye hai! Je, Mungu wako unayemtumikia daima ameweza kukuokoa na simba hawa?” 21. Danieli akamjibu mfalme, “Uishi, ee mfalme!
22. Mungu wangu alileta malaika wake kuvifumba vinywa vya simba hawa, nao hawakunidhuru. Alifanya hivyo kwa sababu alijua mimi sina lawama yoyote kwake na wala sijafanya lolote baya mbele yako.”
23. Hapo mfalme akafurahi sana; akaamuru Danieli atolewe pangoni. Basi wakamtoa, naye alikuwa hajadhurika hata kidogo, kwa sababu alimtegemea Mungu wake.

Hahahaha! Mfalme Dario ananifurahisha jambo moja, alikuwa mwaminifu, anayemjua Mungu japokuwa hakuwa anamuabudu, na mwepesi kutaka suluhu.

Visa hivyo na vingine ambavyo sijavieleza hapa vinatueleza na kutufundisha namna utawalani kulivyo. Kupigwa ni dakika moja tuu.

Hakuna Rais au Mfalme mjanja ambaye hataweza kupigwa za uso na wahuni.
Pona pona ya Marais au wafalme inakuwaga pale wanapoteua watu wenye kumjua Mungu, waaminifu kwa Mungu, watu wapenda haki, na wenye ujasiri wa kumshauri sio vile atakavyo mfalme bali vile ilivyosahihi kushauriwa.

Wito; hata katika maisha ya kawaida tunapofanya teuzi za marafiki, jamaa na hata wenzi wa maisha ni lazima tuzingatie rafiki, jamaa au wenzi wa maisha waliowacha Mungu. Vinginevyo kupigwa kupo nje nje tuu, wahuni ushaambiwa sio watu wazuri.

Kwenye sifa za teuzi, nimeelezea sifa moja tuu ambayo ni HEKIMA, AKILI NA MAARIFA. Sifa zingine nne zilizobakia sijazitaja hapa kwa namna yoyote ile.

Niishie hapa maana kuna watu wangu hawakawii kusema nimeendika andiko refu mno. Ila kama umefika mpaka kusoma hapa nakupa hongera sana kwa maana utakuwa umejifunza mengi. Kazi kwako kufanyia kazi.

Ulikuwa nami;

Robert Heriel
Taikon wa Fasihi
0693322300
Kwa sasa Dodoma
 
Yakifanyika mambo mazuri utasikia: Mh. Rais ni jembe kweli kweli.

Yakifanyika mambo ya hovyo utasikia:Tatizo rais anadanganywa na wasaidizi wake.
kidini na kisheria lawama na pongezi huenda kwa anayetoa maamuzi, yaani Rais au Mfalme.

Ni kosa lake kushindwa kujua njama au hila za washauri wake. Ni heri yake ikwa atashauriwa jambo jema bila kuleta madhara.

Kumbuka wazee wa njama au hila huwadanganyaga viongozi kuwa jambo wanalomshauri ni jema na litapendwa na wengi na hutmpa vithibitisho kabisa, Rais au mfalme akishafanya ndio anajua kuwa aliingizwa mkenge. Hahahah
 
Viongozi ambao ni matured, civilized and educated uwapenda watu wanaowakosoa zaidi na uchukia watu wanaowasifia, thus wameacha legacy kubwa na kuwa viongozi mashuhuru na waliofaulu kwenye uongozi.
 
Naam Mkuu
 
Kazi nzuri ENDELEA[emoji871]
 
Back
Top Bottom