Hata songwe Hela Uviko zimepigwa, mkurugenzi wake yupo kimya

Hata songwe Hela Uviko zimepigwa, mkurugenzi wake yupo kimya

Songwe Yetu

Member
Joined
Nov 22, 2021
Posts
84
Reaction score
99
Nimemskia madam president jana akisikitishwa sana wakurugenzi wanne walioshindwa kusimamia pesa ya uviko kuagiza mamlaka zinazohusika kutengua ukurugenzi wao. Nashauri pia Mhe Rais apate taarifa rasmi za wilaya zote ikiwa pamoja wilaya ya Songwe.

Kwani kuna ubadhirifu mkubwa ulifanywa na wajajanja wachache. Majengo mengi yamepasuka hata kabla hayajaanza kutumika. Madirisha yameegeshwa.

Nilipita sehemu nikakuta mengine yameanza kuibiwa na watu wasiopenda maendeleo.

Ukija kwenye madawati hayajapigwa msasa na waliambiwa wayafanyie marekebisho lakini mpaka sasa hawajafanyia. Cha kusikitisha zaidi waliosimamia shughuli nyingi za ujenzi wa majengo wamehamishwa kwenda vituo vingine na hawajakabidhi majengo.

Huu umekua ni mtindo wa wilaya Songwe.badala ya kuwawajibisha wenyewe wamekuwa wanawahamisha na kule wanakoenda wanabaki na vile vyeo ili wakaharibu na kule.

Tunajenga jamii ambayo ambayo itaharibu kazi pindi inapopewa isimamie.Nina majina ambayo watu walipewa usimamizi wa kazi Serikali na wameharibu kwa makusudi kwa sababu ya upigaji wao na wamehamishwa kupelekwa sehemu nyingine au kupandishwa vyeo.

Mkurugenzi wa wilaya hii amebariki mambo haya na wafanyakazi wanahamishwa. Kwanini asihusishwe na uharamia huu ambao umefanywa na watu hawa. Kwanini amewahamisha kabla hawajakabidhi miradi na kusababisha watoto wetu wakose mahala pakusomea kwa sababu walipopita walisema wanafunzi hawarusiwi kuyatumia madarasa mpaka maboresho walioongelea yafanyike. Waliosimamia wamekimbia hawataki kuja kukabidhi.
 
Viwango vya upigaji vinatofautiana.

Huko walikochukuliwa hatua inamaana walivimbiwa.
 
Back
Top Bottom