kovai tamil taiga
JF-Expert Member
- Sep 28, 2013
- 1,451
- 2,059
Kauli hii inasikika sana kutoka kwa baadhi ya mashabiki,wanachama na hata viongozi wa Yanga.Ukiitafakari kauli hii kwa mbali inaonyesha hali ya mashaka kuwa CCL sio saizi yetu.Hii kauli nashauri isitumike kabisa kwani inashusha morali.CCL ina faida kubwa kuliko shirikisho.Kwa Simba kufika hatua ya robo iliweza kuvuna points 15 ambazo zilitosha kuifanya nchi ya Tanzania kuingiza timu nne kwenye michuano ya CAF tokea dunia iumbwe,Yanga kwa ushiriki wake miaka ya nyuma hasa kombe la shirikisho iliweza kuvuna points 3 tu.Hivyo tuweke lengo la kuitoa Zesco sio vinginevyo