Hata ukibisha kwa sasa, Simba huwezi kuitoa kwenye tatu bora ya Afrika

Hata ukibisha kwa sasa, Simba huwezi kuitoa kwenye tatu bora ya Afrika

Wanatamani hiyo mechi ya mzunguko wa pili wa ligi tarehe 8 ya mwezi Mei, iahirishwe vile!

Ujanja wote wa kucheza ligi ya Mabingwa Afrika huishia wanapokutana tu na timu ya Wananchi na wale wajelajela wa Priaons!
Mkuu Tate kwenye mechi hizo hakuna mpira ila huwa tunacheza na kina bruce lee
 
No labda useme 10 bora
Kwenye msimamo wa jumla kwa timu zote 26 baada ya mechi 5 Simba Ni ya pili nyuma ya Mamelod Sundowns ya Afrika ya kusini!! Upo hapo? Wote Wana point 13, wote goal difference ni 8 lakini Mamelod Sundowns Wana magoli ya kufunga 10 wakati Simba Wana magoli ya kufunga 9. Upo hapo!! Usiumie, habari ndo hiyo! Tatu Bora Simba ndani!!
 
Sawa nimekubali
 
Hao CAF wanatakiwa wajue pia Simba inashika nafasi ya pili kwenye ligi ndani, hivyo watambue kuwa kuna mtemi mwingine anakuja kukinukisha msimu ujao.

Wawe wanaipongeza na Yanga pia, waache upendeleo tutaitisha press wasipoipongeza Yanga kwa kuongoza ligi.
Wanashika nafasi ya pili kwa sababu wana viporo ngoja wamalize viporo uje na kauli yako
 
Anaandika @exaud_msaka_habari

Huwezi kutaja Timu zako tatu bora Africa kwa sasa kwenye haya Mashindano ukaiacha Simba, tukubali tu hilo kwanza ndio tuendelee kijadili soka.

Ukitaka kupima uwezo wa Simba subiri siku wacheze na Mitimu mikubwa kama hii ndio unaweza kupima.

Bonge moja la Mechi leo, utulivu, Malengo, na kuzingatia wanachoambiwa na Mwalimu ndio kinawafanya Simba wawe bora sana Msimu huu.

Mchezaji mmoja mmoja kila mtu ni Bora kwa upande wake, akikuudhi dakika moja basi ujue dakika tatu zijazo atakufurahisha.

Tunaendelea kujifunza Soka kupitia kwa Chama, tunaendelea kujiona hatujui soka kupitia Chama.

Niliwahi kusema hapa mtu anayejua mpira usimtukane hata akifanya kitu gani, anabakia anajua na kuna Siku atakuonesha.

ALL IN ALL DALILI ZINAONESHA SIMBA HAISHII ROBO FAINALI.

View attachment 1742385
Simba ni ya 13 kwa Africa.
Wacha porojo
 
Back
Top Bottom