Cute Wife
JF-Expert Member
- Nov 17, 2023
- 1,906
- 5,000
Wakuu,
Nadhani tutakubaliana pande zote kuwa maji sasa hivi ni changamoto. DAWASA walishauri watu wafunge pump, maji hata yasipokuwa na presha sana inaweza kusaidia!
Arooo, sasa hivi kwanza maji hayatoki, yakitoka ni usiku, halafu presha ni ile ya kuchululu, yaani hata pumzi hazifanyi kazi.
Kwa inavyoonekana hali ni mbaya. Maana hata ukiwatafuta DAWASA unaambiwa tu wamepokea changamoto yako, inashughulikiwa, au wanashughulikia tatizo la kutoa upepo, lakini tatizo hili halijawahi kuisha!
Yaani ni kama kuna jambo wanajua limeharibika lakini hawaelezi watu ukweli. Sasa ni bora waendelee kutudanganya au kutuambia ukweli, kama ni ratiba watu wajue siku fulani na fulani maji yatatoka?
Lakini pia waje watuambie yale maji waliyokuwa wanajitapa tumeyavuna mpaka yaanza kumwagika yako wapi? Pia Watanzania wanafidiwa vipi kwa kukosekana kwa huduma hii muhimu? Maana kama nilivyosema hapa kumradhi haitoshi!
DAWASA Wizara ya Maji