Wote Mko sawa ila Tatizo kuenda Mmoja anaamini kuwa Mleta Mada Kajaribu Kutoa taarifa za Siri au Kuvunja Miiko ya Maadili ya Utumishi kwa kuleta Wazi na kuhoji modality ya Upandishwaji wa Daraja kwa watumishi...
Kwanza kabisa Upandishwaji wa Daraja wa Mtumishi unaongozwa na
Kanuni za Kudumu za Utumishi wa Umma (Standing order for Public servants 2009) kanuni namba D.50 na D.51..
View attachment 3019797
NA Mtu hapandishwi Daraja kama Cohort series au Kwamba walioingia mwaka mmoja au mwezi mmoja wote wanastahili kupanda Daraja kwa kuwa ni Cohort moja..
Appointing Authority itaamua Kama una sifa au Vigezo vya kupandishwa Daraja baada ya Kuona una sifa itapeleka Maombi ya wewe Kuwa approved kupandishwa na itapeleka maombi hayo kwenye Baraza la Madiwani..
Baraza la madiwani likipitisha Basi utapewa Barua ya Kupandishwa Huku ukitakiwa Kuwa ndani ya Uangalizi(Probation) na kama ukivunjs miiko utarudi katika nafadi yako ya Zamani..
NB: Ni marufuku kudai Kupandishwa Daraja kwa HR wako hata kama Ni haki yako, Unaruhusiwa kumkumbusha ila sio Kudai kupanda Daraja hiyo iko chini ya Standing order 2009 (Kanuni za kudumu za utumishi wa Umma) kanuni D53 na D54
View attachment 3019801