Hataki kuzaa kabla ya ndoa

Hataki kuzaa kabla ya ndoa

Kontoro

Senior Member
Joined
Apr 24, 2020
Posts
123
Reaction score
286
Habari wana jf, mimi ni kijana wa miaka 32. Nipo kwenye mahusiono ya miaka 5 na binti wa watu mmoja. Nimekuja hapa jf kuomba ushauri kwa wakubwa zangu wenye uzoefu wa hili jambo maana linanitatiza.

Kipindi tuna miaka 3 kwenye mahusiano, mpenzi wangu alipata mimba ila bila kunipa taarifa aliitoa na taarifa akanipa baada ya kuitoa na nilidhibitisha kama alikuwa nayo na akaitoa. Nilimmind sana na tukakaa kama mwezi bila mawasiliano. Wasiwasi wangu ulikuwa ni kwamba atakuwa ameitoa mimba bila kunishirikisha kwa sababu hataki kuzaa na mimi.

Baadaye aliniomba msamaha na kunieleza historia yake fupi ya ukweli ya maisha aliyokulia. Kalelewa na single mummy, familia yao wamezaliwa watoto wa kike 3 ambao kila mmoja ana baba yake na baba yake hamjui hadi sasa.

Dada zake wote wamezalishwa tuu na hawajaolewa, dada yake mmoja kazalishwa na wanaume 3 tofauti na analea watoto wote mwenyewe na haishi na mume. Na dada mwingine ana watoto 2 naye anawalea bila mume.

Justification ya abortion aliyoifanya ni kutokana na historia ya maisha yake kuwa magumu kwahiyo asingependa mwanae naye akue bila baba kama yeye alivyokua. Na pia historia ya dada zake ambao wote wamezalia kwao kwa hiyo asingependa nayeye awe kama wao. Ilibidi nimwelewe na tukaendelea kudate hadi sasa tuna miaka 5 kwenye mahusiano.

Tangu naanza kudate naye nimemfuatiria sana kujua mienendo yake maana kwenye simu yake nilimwekea program ambayo nimeitengeneza mwenyewe ambayo naweza kusikiliza simu zote anazopiga na kupigiwa, naweza soma message zote anazotuma na kutumiwa, naweza angalia picha zote ambazo zipo kwenye simu yake, naweza soma message za whatsup, fb n.k pia naweza mrekodi sehemu yoyote aliyopo bila yeye kujua. Katika kumfuatiria kote issue ninazokutana nazo ni za kawaida ila sijawahi kuona akiwasiliana na mwanaume mwingine as if anadate naye. In short ni mwaminifu kwangu.

Nimekuja na pendekezo moja kwake na kumwambia kwamba kabla sijakuoa nataka nikupe mimba na uzae kwanza kwa sababu madhara ya kutoa mimba kwa mabinti wengi ni ugumba, au kupata mimba zikatoka. Kwahiyo mimi siwezi kukuoa na ukawa na matatizo hayo ambayo najua ulitoa mimba na hayo matatizo unaweza kuwa nayo so inabidi nikutest nijue kama nikikuoa ntaweza endeleza kizazi changu. Sio nakuoa tunaanza kwenda kwa waganga kutafuta mchawi nani kwanini hushiki mimba au tumalize mahospitali tukitakuta dawa ya uzazi.

Baada ya kumwambia hivyo kakataa katakata, kwamba yeye anataka azae akiwa kwenye ndoa.

Mimi sina wazo baya, wala sitaki kumfanyia uhuni wa kumzalisha na kumkimbia, mimi sina mwanamke mwingine zaidi yake ila wasiwasi wangu ni uzazi.

Mabinti wengi wanamatatizo ya kushika mimba kwa sababu walishatoa mimba kabla ya ndoa. Mimi sitaki kufanya hilo kosa.

Naombeni ushauri ndugu zanguni, je mimi nakosea au niko sahihi au nifanyeje ili mahusiano yaendelee vizuri?
 
Jembe kinje umeongea kila kitu mm na miaka 37 nina watoto 6 na mke wangu nilimkuta ana mmoja jumla tuna watoto 7 nilimzalisha mapacha dabo kama mara 2 jumla na singo mara 2 jumla uzazi wake kazaa mara 5 tu kijana wangu wa kwanza nilimpata nikiwa na umri wa miaka 24 mwaka 2007 kwaiyo sasa kijana mm nakushauri uoe uyo mwanamke mtoto ni majaliwa ya Mungu faza kutoa mimba sio tija wewe Muoe mtoto mtapata uyo binti yuko sahihi %100 oa acha kujaribu mzee nakushauri Muoe kama Kinje alivyosema Over....
Acha mbwembwe wewe...! Maneno meeeeengi 'em" oa miaka 32 unasubiri nini? Oa muendelee kuijaza dunia

121.
 
Tatizo binti nae anapigania nafsi yake kuzaa kabla ya ndoa ni nightmare kwake
Hakuamini,
Kwani siunaweza kwenda kupima hospital sio lazma utesti kwa kumpa mimba Mkuu
Huko Hospital kama anatatizo utajua
.
Umeeleza vyema Sana [emoji95]
 
Mada ndeefu halafu kaandika upupu.
Binti alitoa mimba kwa sababu maisha yake hayaeleweki na hataki historia ya familia yake ijirudie kwake. Na anataka kuzaa ndani ya ndoa Leo unamwambia azae ndiyo umwoe. Unawaza vizuri kweli?

Na asiposhika mimba? Mapenzi yanaisha? Kama mimi ni huyo binti mpaka sasa hivi ningeshakuacha.
Miaka mitano kwenye uchumba mnatafuta degree ya udaktari?
 
Wasikuchanganye hawa fanya moja kubwa Kuliko nenda hospitali mpime nashauri mpime wote then baada ya apo ndio utakua na uhakika..Sawa wapo wanao sema Kupata mtoto ni Majaliwa ila ata Mungu alisha kupa Akili na Utashi wa

kukuongoza...Heshimu sana Hisia zako maana izo ni Mlango wa Sita wa Fahamu..

Iyo Mimba iliyo tolewa unahisi ni yako? usikute sio haikuwa yako ndo maana...kosa hili

Katoa hili nalo kosa maana huenda likasumbua kwenye kupata mtoto kama hisia zako zinavyo kutuma.
 
Je kama wewe ndio ungekuwa mwanamke uko tayari uzalishwe nje ya ndoa?

"Fᵒˡˡᵒʷ ᵉˣᶜᵉˡˡᵉⁿᶜᵉ ˢᵘᶜᶜᵉˢˢ ʷⁱˡˡ ᶜʰᵃˢᵉ ᵖᵃⁿᵗˢ ᵈᵒʷN"
 
Hakuna sababu inayoweza kuhalalisha uuaji wa kiumbe kisichokuwa na hatia, hiyo pekee inamfanya akose sifa ya kuwa mke mwema.

Tendo la ndoa ni kwa ajili ya wanandoa. Huo utoaji mimba ni moja ya madhara ya kufanya tendo la ndoa nje ya ndoa. Muoe.

Watoto ni zawadi kutoka kwa Mungu. Mungu akipenda kuwazawadia ni sahihi, asipopenda pia, yupo sahihi.

Ninasisitiza, tendo la ndoa ni kwa ajili ya wanandoa tu.
 
Kuna hatua ndogo bado hujakamilisha ili binti aweze kukuamini na kukuzalia mtoto, inawezekana kwa sasa hutaki ndoa labda kwa sababu za kiuchumi au nyinginezo.

Unaweza kufanya yafuatayo ili kufanikisha lengo lako;

1. kajitambulishe kwao

2. Weka mazingira wazazi wenu wafahamiane

3. Mchukue binti muishi naye pamoja

4. Mshirikishe kwenye mipango ya maendeleo yako huku na yeye akitekeleza.

5. Hapo atakuzalia hata wewe usipohitaji na hata tendo atakuwa anakuachia ujipimie unavyotaka
 
Mmhh
 
Habari wana jf, mimi ni kijana wa miaka 32. Nipo kwenye mahusiono ya miaka 5 na binti wa watu mmoja. Nimekuja hapa jf kuomba ushauri kwa wakubwa zangu wenye uzoefu wa hili jambo maana linanitatiza.

Kipindi tuna miaka 3 kwenye mahusiano, mpenzi wangu alipata mimba ila bila kunipa taarifa aliitoa na taarifa akanipa baada ya kuitoa na nilidhibitisha kama alikuwa nayo na akaitoa. Nilimmind sana na tukakaa kama mwezi bila mawasiliano. Wasiwasi wangu ulikuwa ni kwamba atakuwa ameitoa mimba bila kunishirikisha kwa sababu hataki kuzaa na mimi.

Baadaye aliniomba msamaha na kunieleza historia yake fupi ya ukweli ya maisha aliyokulia. Kalelewa na single mummy, familia yao wamezaliwa watoto wa kike 3 ambao kila mmoja ana baba yake na baba yake hamjui hadi sasa.

Dada zake wote wamezalishwa tuu na hawajaolewa, dada yake mmoja kazalishwa na wanaume 3 tofauti na analea watoto wote mwenyewe na haishi na mume. Na dada mwingine ana watoto 2 naye anawalea bila mume.

Justification ya abortion aliyoifanya ni kutokana na historia ya maisha yake kuwa magumu kwahiyo asingependa mwanae naye akue bila baba kama yeye alivyokua. Na pia historia ya dada zake ambao wote wamezalia kwao kwa hiyo asingependa nayeye awe kama wao. Ilibidi nimwelewe na tukaendelea kudate hadi sasa tuna miaka 5 kwenye mahusiano.

Tangu naanza kudate naye nimemfuatiria sana kujua mienendo yake maana kwenye simu yake nilimwekea program ambayo nimeitengeneza mwenyewe ambayo naweza kusikiliza simu zote anazopiga na kupigiwa, naweza soma message zote anazotuma na kutumiwa, naweza angalia picha zote ambazo zipo kwenye simu yake, naweza soma message za whatsup, fb n.k pia naweza mrekodi sehemu yoyote aliyopo bila yeye kujua. Katika kumfuatiria kote issue ninazokutana nazo ni za kawaida ila sijawahi kuona akiwasiliana na mwanaume mwingine as if anadate naye. In short ni mwaminifu kwangu.

Nimekuja na pendekezo moja kwake na kumwambia kwamba kabla sijakuoa nataka nikupe mimba na uzae kwanza kwa sababu madhara ya kutoa mimba kwa mabinti wengi ni ugumba, au kupata mimba zikatoka. Kwahiyo mimi siwezi kukuoa na ukawa na matatizo hayo ambayo najua ulitoa mimba na hayo matatizo unaweza kuwa nayo so inabidi nikutest nijue kama nikikuoa ntaweza endeleza kizazi changu. Sio nakuoa tunaanza kwenda kwa waganga kutafuta mchawi nani kwanini hushiki mimba au tumalize mahospitali tukitakuta dawa ya uzazi.

Baada ya kumwambia hivyo kakataa katakata, kwamba yeye anataka azae akiwa kwenye ndoa.

Mimi sina wazo baya, wala sitaki kumfanyia uhuni wa kumzalisha na kumkimbia, mimi sina mwanamke mwingine zaidi yake ila wasiwasi wangu ni uzazi.

Mabinti wengi wanamatatizo ya kushika mimba kwa sababu walishatoa mimba kabla ya ndoa. Mimi sitaki kufanya hilo kosa.

Naombeni ushauri ndugu zanguni, je mimi nakosea au niko sahihi au nifanyeje ili mahusiano yaendelee vizuri?
Hapo kwenye upelelezi tu tayari nimekuona sio, sasa kama unasikiliza simu zote, msg zote, sijui fb ,sijui nini, inamaanisha huyo dada hana privacy hata kama anaongea na mama ake na ndugu zake wewe unajua 😏😏😏Inaonyesha wewe unamatatizo mengi na huyo dada anakuvumilia sana.
Ushauri; nendeni hosp mkapime vizazi na sio kung'ang'ania kumtest kwa kumpa mimba. Alaf ukute wewe ndio hauna uwezo wa kuzalisha 😂😂😂
utajinyea
 
Back
Top Bottom