Wadau wa JamiiForums, habari zenu.
Jana, Machi 26, 2026, Tume ya Ulinzi wa Taarifa Binafsi (PDPC) ilitoa tangazo ambalo linataka kila mtu au taasisi inayokusanya na kuhifadhi taarifa za watu kujisajili ifikapo Aprili 8, 2026.
Ingawa lengo la Sheria hii (PDPA, Sura ya 44) ni zuri—kulinda faragha na haki zetu za kidijitali—mtindo uliotumika wa "kufagia wote" (blanket approach) bila kujali ukubwa wa biashara, pamoja na ada kubwa sana za usajili zinazolalamikiwa, ni hatari sana. Hatua hii inaweza kuua biashara ndogo, kuminya uhuru wa habari, na kutugeuza kitega uchumi badala ya kutulinda.
Tangazo lao ni hili:
Hapa chini nimechambua kwa lugha rahisi kwanini tangazo hili ni baya kwa mwananchi wa kawaida na nini kifanyike:
Pia:
Naomba mamlaka zirekebishe tangazo hili mara moja!
Nini maoni yenu wadau?
Jana, Machi 26, 2026, Tume ya Ulinzi wa Taarifa Binafsi (PDPC) ilitoa tangazo ambalo linataka kila mtu au taasisi inayokusanya na kuhifadhi taarifa za watu kujisajili ifikapo Aprili 8, 2026.
Ingawa lengo la Sheria hii (PDPA, Sura ya 44) ni zuri—kulinda faragha na haki zetu za kidijitali—mtindo uliotumika wa "kufagia wote" (blanket approach) bila kujali ukubwa wa biashara, pamoja na ada kubwa sana za usajili zinazolalamikiwa, ni hatari sana. Hatua hii inaweza kuua biashara ndogo, kuminya uhuru wa habari, na kutugeuza kitega uchumi badala ya kutulinda.
Tangazo lao ni hili:
Hapa chini nimechambua kwa lugha rahisi kwanini tangazo hili ni baya kwa mwananchi wa kawaida na nini kifanyike:
1. Hatari kwa Wananchi na Jamii
- Kuminya Uhuru na Kufuatiliwa (Surveillance): Sheria inataka Asasi za Kiraia (NGOs), Vyombo vya Habari, na Vyama vya Siasa visajiliwe na kutoa "ripoti za kila robo mwaka". Bila ulinzi imara wa kisheria, Serikali kupitia Tume hii inaweza kutumia mwanya huu kufuatilia taarifa za Waandishi wa Habari, Wafichua Maovu (whistleblowers), na wakosoaji wa Serikali bila sababu za msingi.
- Kuuwa Biashara Ndogo Ndogo: Tangazo hili linajumuisha kila sekta. Hii inaweza kutafsririwa kuwa hata "Kampuni ndogo ya Usafi", "Lodge/Gesti ya mtaani" au "Duka la rejareja" inatakiwa kujisajili na kulipa ‘mamilioni’. Hii itafanya biashara nyingi ndogo zishindwe kujiendesha na kufungwa, au kurudi kufanya kazi zisizo rasmi mitaani ambako hakuna ulinzi wowote wa taarifa za wateja.
- Kutengeneza Sehemu Rahisi ya Kudukuliwa (Honeypot): Kulazimisha kila biashara nchini kutuma taarifa zao za kiutendaji kwenye mfumo mpya wa Serikali (RCMIS) kunatengeneza kanzidata moja kubwa sana. Endapo mfumo huu wa PDPC utakuwa hauna ulinzi wa kutosha wa kimtandao, wadukuzi wanaweza kuiba taarifa za nchi nzima kwa mkupuo na kutuweka Watanzania wote hatarini.
2. Kupitiliza Mipaka na Kukosekana kwa Usawa
Sheria nzuri za kisasa huzingatia ukubwa wa hatari (Proportionality). Huwezi kulinganisha chama cha ushirika cha wakulima kijijini na kampuni kubwa ya simu (Mitandao ya Simu).- Matakwa Yasiyotekelezeka: Kuwataka wafanyabiashara wadogo, wamachinga, mafundi, waandishi wa kujitegemea na vikundi vidogo kuajiri "Ofisa wa Ulinzi wa Taarifa (DPO)" na kununua mifumo ya gharama ya ulinzi ni kupitiliza na kuwaonea watu.
- Makundi haya madogo yalipaswa kusamehewa (Exemptions) kwenye hili takwa la lazima.
3. Dunia Inafanyaje? (Mifano Bora)
Tanzania inaonekana kwenda kinyume na taratibu za kimataifa:- Mfano wa Kenya: Hapa jirani, nchini Kenya, huwezi kulazimishwa kusajiliwa mpaka mapato yako yafikie kiwango fulani (k.m. Tsh Milioni 90) au unahudumia watu zaidi ya 10,000. Sio kila mwenye duka anasajiliwa!
- Kulinda Wanahabari: Sheria za Ulaya (GDPR) na Afrika Kusini (POPIA) zinatoa misamaha maalum kwa waandishi wa habari na kazi za sanaa ili kulinda uhuru wa habari. Sisi tumewaweka kundi moja na mabenki.
- Maofisa wa Taarifa (DPO): Kuajiri DPO inapaswa iwe ni lazima kwa taasisi kubwa tu, zinazokusanya taarifa nyeti sana za watu. Kulazimisha kila biashara iwe na DPO ni jambo lisilowezekana kwani hata wataalamu wenyewe nchini hawatoshi.
4. Kwanini PDPC Inapaswa Kusitisha Agizo Hili Haraka?
- Tozo Kama Kodi Mpya: Kulazimisha ada kubwa za usajili kwa biashara ndogo na taasisi zisizo za kiserikali ni sawa na kuwatoza kodi mpya yenye lengo la kukusanya mapato, wala si kulinda faragha za watu.
- Muda Mfupi Usiowezekana: Kuwapa watu siku chache (hadi Aprili 8, 2026) wawe wametekeleza haya yote ni haiwezekani. Lengo linaonekana ni kutega watu washindwe ili wapigwe faini za kutisha (hadi Tsh Bilioni 5) badala ya kutoa elimu.
5. Nini Kifanyike?
PDPC inapaswa kuanza na mtindo wa “Awamu”, ambapo italenga taasisi kubwa tu (Kampuni za Simu, Benki, Hospitali kubwa).Pia:
- Elimu kwa Umma na Asasi za Kiraia: Vyombo vya habari na Asasi za Kiraia pigieni hili kelele. Elezeni umma jinsi utaratibu huu utafunga zahanati za mitaani na vyama vya ushirika. Faragha isiwe bidhaa ya anasa au kodi onevu.
- Bunge Liingilie Kati Mjadala: Kamati ya Bunge ya Miundombinu inapaswa kuingilia katika katika hili suala haraka na kupitia upya hizi tozo na kanuni kandamizi.
- Kutumia Mahakama: Kama PDPC itang'ang'ania, nashauri asasi za kiraia zijiandae kwenda Mahakama ya Afrika Mashariki (EACJ) au Kamisheni ya Haki za Binadamu kuomba zuio dhidi ya ukandamizaji huu.
Naomba mamlaka zirekebishe tangazo hili mara moja!
Nini maoni yenu wadau?