A
Anonymous
Guest
Wanafunzi wa Chuo cha Ustawi— Institute of Social Work, Bamaga, Dar es Salaam wanalalamika ratiba za masomo zinazoenda mpaka Saa 4 Usiku. Hii inahatarisha usalama wao hasa wakati wa kurudi makwao huku wengine wakitokea mbali kama vile Gongo la Mboto, Mbagala, Tegeta; hii inapelekea kufika makwao sio chini ya Saa 6 Usiku.
Kero hii imeleta shida kwa wazazi na baadhi ya wanafunzi wa kike kudai kuwa wanahofia vitendo vya ubakaji na ukatili mwingine ikiwemo uhalifu nyakati za usiku.
Pia, soma: √ - Chuo cha Ustawi wa Jamii: Wanafunzi wanachagua wenyewe kusoma asubuhi au Mchana, tunawashauri wakae karibu na Chuo
Tunaomba uongozi wa chuo hiki kufuatilia jambo hili na kuweka ratiba vizuri. Vyuo vingine muda wa masomo mwisho saa 2 usiku.