KERO Hatari kwa usalama wa wanafunzi chuo cha Ustawi—DSM: Ratiba ya masomo hadi saa 4 usiku

KERO Hatari kwa usalama wa wanafunzi chuo cha Ustawi—DSM: Ratiba ya masomo hadi saa 4 usiku

Hii ni kero ambayo mwananchi ameiwasilisha JF akitaka wahusika kuchukua hatua
Wanafunzi wa Chuo cha Ustawi— Institute of Social Work, Bamaga, Dar es Salaam wanalalamika ratiba za masomo zinazoenda mpaka Saa 4 Usiku. Hii inahatarisha usalama wao hasa wakati wa kurudi makwao huku wengine wakitokea mbali kama vile Gongo la Mboto, Mbagala, Tegeta; hii inapelekea kufika makwao sio chini ya Saa 6 Usiku.

Kero hii imeleta shida kwa wazazi na baadhi ya wanafunzi wa kike kudai kuwa wanahofia vitendo vya ubakaji na ukatili mwingine ikiwemo uhalifu nyakati za usiku.

Tunaomba uongozi wa chuo hiki kufuatilia jambo hili na kuweka ratiba vizuri. Vyuo vingine muda wa masomo mwisho saa 2 usiku.
Nchi zinazojielewa masomo mwisho saa 11 jioni
 
Nimewahi kusoma kabla chuo hiko. Sio kana kwamba ratiba inaisha usiku bali ni maamuzi ya mwanafunzi mwenyewe kusoma asubuhi ama usiku.. Ratiba hiyo iliweka ili kusave wale wenye kazi zao mchana au majukum mbal mbal nao waweze kupata haki ya kusoma..
Ikiwa mtu angekuwa na tatzo hilo basi angebadilsha mwenyewe.
Mtanikosoa kama sipo sahihi..
Sahihi, umemaliza
 
Point 📌
 
Back
Top Bottom