Hatari na nusu panzi kutoka kuzimu

bahati93

JF-Expert Member
Joined
Aug 6, 2015
Posts
1,334
Reaction score
2,463
NDUGU WATANZANIA NOMAAAA SANAA

Picha lenyewe linaanza mi nipo zangu natembea kuelekea kituoni. Hii barabara nayotembea ni ya changalawe na kando yake kuna wigo wa block mrefu sana kwenda juu na juu ya huu wigo kuna nyaya za Senyenge kwa msisitizo. Kwa kuwa jua ni kali sana kipindi hichi cha vuli na kwa mimi mpita njia ili kupata kivuli nikaacha barabara kubwa na kuvamia kinjia chembamba pembeni mwa huo ukuta mrefu ambao kwa namna moja uliweka kivuli kwenye miguu yake. Ikanibidi kuruka nyasi na miba iliyokuwa katikati ya barabara na kutua kwenye hii barabara nyembamba ya waenda kwa miguu sasa nikawa sina shida na jua tena, nikarelaxy nikawa naenda taratibu.

Wakati natembea, nikatazama mbele nikaona ukuta unaonihifadhi kwa kivuli umekunja kushoto na kivuli kikawa ndo mwisho wake. Kwa kweli nilivyoingia juani nikawa nimehamaki ikanibidi nivuke barabara ya changarawe niingie upande wa kulia yake. Mara paa nikashuhudia kwa macho yangu mwenyewe vitu vyeusi vyenye uhai.kwa hakika vilikuwa viumbe wa kutisha sana. Kwanza ni vyeusi tii kuanzia miguu mpaka matumbo yao. Niliogopa sana, nikawatizama nikagundua ni panzi, tunutu inatisha sana kuona tunutu mweusi tena mchana, wakati nawashangaa mmoja akaruka kwa kufyatua miguu yake.... YESUUU NAKUFAAA! nililia kwa sauti kuu, na nisione msaada wowote karibu nami. Kuogopa kwangu kulipelekea kurudi nyuma bila hesabu hivyo kupelekea kujikwaa na kuanguka kwa kukaaa chini. Cha ajabu vile viumbe vilibaki pale na kuendelea na shughuli zao wala havikutawanyika. Ndipo kwa mbali nikakiona kimoja nadhani bila shaka ndio kiongozi chao kina mwili wa panzi na KICHWA cha mbuzi cheusi. Nikafanya kujiburudha nisije dhuliwa na nikajishauri nivipige picha kama ushaidi endapo nitazuriwa.

 
Umesahau kumalizia hapo chini kuwa "nikashtuka usingizini kumbe ilikuwa ndoto ya mchana"
 
Eti ushahid hahaha
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…