HATARI : Tiba za asili za Kichina sasa zagundulika kuchanganywana dawa za kuulia wadu

HATARI : Tiba za asili za Kichina sasa zagundulika kuchanganywana dawa za kuulia wadu

kbm

JF-Expert Member
Joined
Oct 5, 2012
Posts
5,224
Reaction score
1,677
dawa.jpg


*.Kati ya bidhaa 36, zilizonunuliwa 32 kati yake zilikuwa zina chembechembe aina tatu za dawa hizo za kuulia wadudu.
*.17 kati yake zina chembechembe za dawa za kuulia wadudu zilizoanishwa na shirika la Afya duniani (WHO).

Dawa hizi zimekuwa zikitumika katika nchi mbalimbali kwa sasa
Licha ya kuaminiwa na kuchukuliwakama tiba bora zaidi nchini, imegunduliwa kuwa dawa za mitishamba za Kichina zina chemchembe za dawa za kuulia wadudu.
Uchunguzi uliofanywa kupitia dawa hizo zilizonunuliwa katika maduka mbalimbali yanayouza dawa hizo nchini Uingereza umebaini kuwa dawa hizo zina kemikali zenye sumu zinazotokana na dawa za kuulia wadudu.
Pamoja na ukweli kuwa kemikali hizo zipo kwa kiasi kidogo sana , inasemekana matumizi ya dawa hizo kwa muda mrefu yanasababisha uharibifu katika Vichocheo, matatizo katika mfumo wa uzazi kwa wanaume na uharibifu wa mimba.
Zaidi ya Waingereza milioni tatu hutumia dawa za Kichina kujitibu kwa maradhi mbalimbali kila mwaka.
Katika kipindi cha miezi sita kuanziaNovemba 2012 hadi Aprili 2013, wachunguzi wa Greenpeace walinunua aina saba tofauti za dawa za mitishamba zilizoingizwa kutoka China kwa ajili ya kuzifanyia majaribio.
Dawa hizo zilinunuliwa kutoka kwa wauzaji wa rejareja kutoka kwenyenchi saba tofauti ikiwamo Uingereza.
Dawa hizo ni miongoni mwa zile zinazoaminiwa zaidi na wauzaji hao na pia zinadaiwa kuwa tiba halisi ya magonjwa sugu ambayo yamekuwa wakiwasumbua watu wengi hususan katika jamii ya Waasia.
Sampuli 26 kati ya 29 zilizochukuliwa kutoka Uingereza na maduka mengine barani Ulaya ziligundulika kuwa kuna chembechembe za dawa za kuulia wadudu.
Sampuli moja ya ‘honeysuckle’peke yake ilinunuliwa nchini Uingereza ilikuwa na viashiria 17 vya dawa hiyo ya kuulia wadudu, inayozidi nane katika kiwango cha usalama cha Ulaya
Akitoa maoni yake kuhusiana na utafiti huo, mwanasayansi mkuu waTaasisi Greenpeace ya Uingereza, DkDoug Parr, alisema‘Sumu zilizoko kwenye dawa hizi za kichina zinahatarisha afya za watumiaji wa dawa hizo”
Watu wanaotumia dawa hizi kwa kuamini kuwa zinaponya haraka na kuboresha afya zao, washtuka sana kusikia kuwa dawa walizokuwa wakitumia kwa muda mrefu zina hatari na athari kubwa kwa afya zao. ‘Serikali ya Uingereza na Umojawa Ulaya kwa ujumla wanatakiwa kuboresha mfumo wao wa uchunguzi wa usalama wa bidhaa kutoka China, ili kuwanusuru watumiaji wake.

Kati ya bidhaa 36, zilizonunuliwa 32 kati yake zilikuwa zina chembechembe aina tatu za dawa hizo za kuulia wadudu.
17 kati yake zina chembechembe zadawa za kuulia wadudu zilizoanishwa na shirika la Afya duniani (WHO).
Elizabeth Salter Green, Mkurugenzi wa CHEM Trust anasema: ‘ NchinI Uingereza , dawa za kichina zimekuwa zikiaminika kuwa ni asili na zenye afya. Hivyo inashtua sana kusikia eti nyingi kati yake zimeongezewa na chemchembe zenye sumu ndani yake.
‘Tafiti zimeonyesha ni kwa jinsi gani dawa hizi za kichina zima madhara kwa afya za wanaume na hata wanawake”
‘Serikali ya Uingereza inatakiwa kuchukua hatua madhubuti za kuhakikisha kuwa mamlaka zote zinazohusika na ukafuzi wa dawa hizo zinafanya kazi yake ipasavyo ilikulinda afya za watumiaji wa dawa hizi.
Upandaji mbaya : Sampuli ya mmea wa ‘honeysuckle’ iliyonunuliwa nchini Uingereza ilikutwa na chemchembe 17 za dawa ya kuulia wadudu.
Msemaji wa wakala wa udhibiti wa dawa na afya alisema ‘kuna baadhi ya dawa za kichina nchini Uingerezaambazo pengine zimetengenezwa katika viwango vidogo vya ubora aukwa bahati mbaya zimeingiziwa sumu ama viungo haramu.
‘Bidhaa hizi zina hatari sana kiafya na pia si rahisi kuzitofautisha na zilezilizotengenezwa kwa viwango vinavyokubalika kiusalama.
Dk Kaicun Zhao, rais wa chama cha dawa za asili za kichina nchini Uingereza alisema,
“Tungesoma hili kwa kina, pamoja na kufikiria kuwa inawezekana hii haihusishi dawa zote zinazoingia kutoka China ndani ya soko la Uingereza na Ulaya kwa ujumla, kitu muhimu tunachokiona hapa ni kusimamia viwango vya ubora vya dawa hizi
‘Ni matumaini yetu kuwa Uingereza na Ulaya kwa ujumla wataharakisha kuanzisha utaratibu sahihi wa upimaji wa viwango vya ubora katika dawa za mitishamba hususani dawa za Kichina”.

Chanzo: MCL
 
Mkuu.@kbm Hongera kwa kutupa Habari nzuri kabisa jamani tumieni dawa zangu za Tiba Mbadala, hazina madhara yoyote yale muacheni huyo Mchina anataka kuwamaliza Watu taratibu asanteni. Kwa wenye shida mbali mbali ziliozoshindikana kutibiwa Hospitalini awasiliane na mimi kwa barua ya pepe Address yangu hii hapa fewgoodmana@hotmail.com
 
Back
Top Bottom