Hatari ya kampuni nyingi kufutiwa usajili

M. Mwakalonge

Member
Joined
Dec 2, 2012
Posts
49
Reaction score
4
Kwa Mujibu wa sheria ya makampuni ya mwaka 2002, vifungu vya 128, 132 na 438 kila kampuni iliyosajiliwa Tanzania inawajibika kupeleka taarifa za mwaka ikiwa ni pamoja na taarifa za mahesabu yaliyokaguliwa kwa msajili wa makampuni (BRELA). Serikali kupitia BRELA wametoa tangazo kwa makampuni yote yapeleke taarifa zao, Mwisho wa kufanya hivyo ni Tarehe 31 December 2014. Kushindwa kufanya hivyo ni kuvunja sheria, wamiliki na wakurugenzi watafikishwa mahakamani au kampuni kufutiwa usajili au vyote kwa pamoja.
Waone Anjoa Company Limited (Business Consultancy Company) kwa huduma na ushauri kuhusinana na suala hili.
Wasiliana nasi kwa,

  • Simu: 0759-692024 au 0688-510564
  • Email: info@anjoa.co.tz au anjoa_limited@yahoo.com
  • WatsApp: 0759-692024
  • Au fika ofisini kwetu, Dar es Salaam, Kinondoni – Manyanya, Togo street, plot number 336, ghorofa ya pili, Jengo lililo karibu na Togo tower.
 
Hiyo ni kweli. Ni vizuri wamiliki wa makampuni wakalizingatia hilo.
 
Naona unaandika na kujicomentia mwenyewe! Tatizo lenu ni moja tu, pricing imewashinda mna tamaa sana ya pesa.
Bei zenu zipo juu mno na kibaya hamsikilizagi wateja mkishataja mmeta. Mnadhani mnaofanya consultation ni nyinyi wenyewe! Hahaha mtajicommentia sana, wapo watu wanafanya bei nzuri reasonable hapa Dar ndo tunaenda huko siku hizi. shauri yenu Yeboo nkosi
 

Afadhali umewapa za usoni wana tamaa sana hawa jamaa
 
em tumsubiri mhucka wa anjoa arud kwa utetezi juu ya hiz tuhuma

Na hili ni tatizo kwa watoa huduma wa TZ wanataka watajirikie kwa mteja mmoja, matokeo yake wanapoteza wateja wengi .
 
Na hili ni tatizo kwa watoa huduma wa TZ wanataka watajirikie kwa mteja mmoja, matokeo yake wanapoteza wateja wengi .

Yaani.kukuandalia memorandum tu atakuambia umpe laki sita.,, halafu wanacopy na kupest.. Hawa maconsultant tamaa mbele.
 


Ndugu wana JF, ni bora zaidi kusema kitu ulichokifanyia utafiti kuliko kusema jambo ambalo hulijui kabisa. Gharama zetu ni nafuu sana ukifananisha na consultants wengine. Hatujawahi hata sikumoja kutoza mteja bei ambazo zinatajwa na huyu bwana anayejiita "Majaribu 2013" na kwa kazi anayoitaja. Pia hatujawahi kupata malalamiko kwa wateja wetu kuhusu huduma zetu, badala yake tumepokea watu wengi sana ambao walijaribu kufanyiwa kazi na vishoka na mwishowe kutapeliwa. Tuna list ya watu waliojaribu kutafuta urahisi zaidi ya huu tunaowapatia wakaishia kupoteza pesa zao bila mafanikio, Anjoa Co. Ltd ikawa ( imekuwa na itakuwa) suruhisho la matatizo yao. Tunapenda mwenye hayo malalamiko atoe ushahidi, tena ni vizuri yakawekwa wazi hapa ili kila mwana JF aone. Mwisho tungependa kuwashukuru wan JF wote.
 

Mimi malalamiko yangu yapo hapo pekundu.
 

Mimi ni mteja wako mtarajiwa, nikuombe usikimbie sana unapoandika,siku nyingine utaandika matusi bure.
 


Acheni uongo. Wekeni bei zenu wazi hapa zote, kuanzia kusajili NGo mpaka makampuni. Waongo wakubwa nyinyi
 
Kama wewe ni mtafiti nzuri utakuwa umegundua kitu kikubwa sana kwenye hii post. Mtu wa kwanza kujibu hakuweza kuhoji kasoro yoyote ya uandishi, wa pili akaona maneno matatu na wa tatu akaona maneno ya nyongeza mawili. Mpaka sasa hatujapata malalamiko mengine kuhusiana na huduma zetu, pia mlalamikaji kashindwa kutoa ushahidi wowote. Anjoa Co. Ltd tupo na tutakuwepo ili tukuhudumie. Karibu Anjoa Co. Ltd.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…