Hatari ya kutoweka kwa ndizi Bukoba (matoke) Mkoani Kagera, Je, Wizara ya Kilimo ina mikakati ipi?

Hatari ya kutoweka kwa ndizi Bukoba (matoke) Mkoani Kagera, Je, Wizara ya Kilimo ina mikakati ipi?

John Haramba

JF-Expert Member
Joined
Feb 4, 2022
Posts
379
Reaction score
1,412
Kwa miongo kadhaa, ndizi Bukoba zimekuwa zaidi ya chakula kwa wakazi wa Mkoa wa Kagera; zimekuwa msingi wa maisha, utamaduni na uchumi wa jamii nzima. Hata hivyo, nyuma ya taswira ya zao hili lililodumu kizazi hadi kizazi, kuna mabadiliko hatarishi yanayoendelea mashambani na katika mifumo ya uzalishaji, mabadiliko ambayo uenda yakipuuzwa yanaweza kubadilisha kabisa mustakabali wa zao hili la kihistoria.

Katika muktadha huo, matoke maarufu yanayojulikana kama “ndizi Bukoba” yamekuwa alama ya utambulisho wa Mkoa wa Kagera kwa muda mrefu, si tu ndani ya nchi bali hata nje ya mipaka ya Tanzania, yakihusishwa na historia, maisha ya kila siku na hadhi ya jamii inayoyalima.

Hata hivyo, uchunguzi nilioufanya katika Mkoa wa Kagera hasa katika Wilaya za Missenyi, Bukoba Vijijini na Muleba unabaini kupungua kwa kasi kwa uzalishaji wa ndizi Bukoba. Eneo ambalo limebakia na unafuu ni Karagwe na Kyerwa ambapo upatikanaji wa mbolea bado ni rahisi ikilinganishwa na maeneo mengine ya Mkoa huo.

Katika maeneo tajwa kwa sasa familia nyingi zimeanza kutegemea vyakula vingine tofauti na vile vilivyozoeleka, huku mashamba yaliyokuwa yakijulikana kwa migomba mizuri yakiendelea kupotea au kudhoofika.

Baadhi ya changamoto zinabainika...
Uchunguzi wa kimazingira unaonesha kuwa awali kilimo cha ndizi kilistawi kwa kiasi kikubwa kwa kutegemea mbolea ya asili. Wastani wa kaya 7 kati ya 10 zilikuwa na mifugo, hususan ng’ombe, waliokuwa wakizalisha mbolea. Hata hivyo, hali imebadilika; kwa sasa, kati ya kaya 10, ni kaya moja tu yenye mifugo inayoweza kuzalisha mbolea.

Kupungua huku kwa upatikanaji wa mbolea kumechangia kwa kiasi kikubwa kushuka kwa uzalishaji wa ndizi. Kaya chache zinazomiliki mifugo bado zina nafuu katika uzalishaji ikilinganishwa na kaya zisizo na mbolea.

Hata hivyo, katika jamii hizi kuna sababu kadhaa zinazochangia kushuka kwa shughuli za ufugaji:

Kupungua kwa maeneo ya malisho
Katika Mkoa wa Kagera, hususan wilaya zilizohusishwa na uchunguzi huu, kumebainika kupungua kwa maeneo ya malisho kutokana na uwekezaji mkubwa katika kilimo cha miti aina ya pine.

Ongezeko la uwekezaji huo limeenda sambamba na matumizi holela ya madawa ya kuua wadudu pamoja na kuharibu mimea mingine inayochukuliwa kuwa kikwazo kwa ustawi wa miti hiyo.

Aidha, maeneo mengi ya malisho yamechukuliwa rasmi na Serikali kwa ajili ya uhifadhi, huku pia kukiibuka wawekezaji wanaochukua maeneo makubwa ya tingatinga ambayo awali yalitumika kwa ufugaji. Hali hii imepunguza maeneo ya malisho na hivyo kupunguza hamasa ya ufugaji kwa wananchi.

Ukosefu wa elimu ya ufugaji wa kisasa
Ufugaji unaozoeleka katika Mkoa wa Kagera ni ufugaji wa kuchunga katika maeneo ya wazi ya malisho. Wafugaji wanaotumia mbinu za kisasa ni wachache sana. Hali hii inatokana na uhaba wa elimu na maarifa mapya yanayoendana na mabadiliko ya dunia, huku wengi wakiendeleza ufugaji wa kurithi bila maboresho.

Katika maeneo machache ambako ufugaji wa kisasa unafanyika, upatikanaji wa mbolea ni mkubwa zaidi na wa uhakika.

Kukosekana kwa mbolea mbadala
Kwa muda mrefu, uzalishaji wa ndizi katika Mkoa wa Kagera umekuwa ukitegemea mbolea inayotokana na mifugo moja kwa moja. Utegemezi huu umekuwa kikwazo kikubwa pale uzalishaji wa mbolea hiyo unapopungua.

Kwa sasa, hakuna mbolea mbadala inayowafikia Wakulima wengi wa ndizi na ambayo ingeweza kuwa suluhu katika kipindi hiki cha upungufu wa mbolea ya asili.

Mamlaka zinawaza nini?
Ombwe hili linaacha maswali makubwa kwa wataalamu wa Wizara ya Kilimo hususani watafiti: Je, changamoto hii wameiona? Na kama imeonekana, ni kwa nini hakuna jitihada za dhati za kuzalisha na kusambaza mbolea mbadala pamoja na kuhamasisha elimu ya ufugaji wa kisasa?

Kwa hali ilivyo sasa, endapo hakutakuwa na njia mbadala na suluhu za haraka, kilimo cha ndizi kitaendelea kupungua kwa kasi. Hali hii inaweza kubadili kabisa mfumo wa maisha na tamaduni za jamii ambazo kwa muda mrefu zimeitegemea ndizi kama zao kuu la chakula na utambulisho wao.

Kwa kuhitimisha, ushahidi uliokusanywa katika uchunguzi huu unaonesha wazi kuwa kuporomoka kwa kilimo cha ndizi Bukoba si tukio la kawaida bali ni matokeo ya mabadiliko ya kijamii, kiuchumi na kisera ambayo hayajaambatana na suluhu mbadala.

Endapo hakutakuwa na hatua za makusudi za kuimarisha ufugaji wa kisasa, kuhakikisha upatikanaji wa mbolea mbadala na kulinda rasilimali za uzalishaji, Mkoa wa Kagera uko hatarini kupoteza zao la chakula, chanzo cha kipato na sehemu muhimu ya utambulisho wa jamii yake.

Makala hii itaendelea sehemu ya pili...
 
Kilimo ni Biashara, Sasa jiulize watu huko hawaoni gaida kulima? Mbolea inaweza fuatwa hata Kahama kama mtu anataka kuwekeza kweli, tupunguze mindset za ujamaa,
Yaani samadi ifuatwe kuvuka mikoa, gharama za usafirishaji umezitathimini?

Nadhani mtoa mada tumpe shime kwa kuibua hoja hii mtambuka.
 
Wakazi wa mkoa huo hasa maeneo ya wilaya za Missenyi na Bukoba Vijijini wapige chini zao la ndizi kabisa kabisa, wafanye mambo mengine.

Kwanza kuna Panama disease ambao huu ugonjwa hao fungus wanakaa ardhini kwa miaka hadi 200. Sasa mnarudisha lini ardhi kwenye usawa?
Na ukizingatia ecology ya hayo maeneo ina carriers wa hiyo fungus.

Ugonjwa wa mnyauko ndio huo nao unaharibu kabisa uzalishaji.

Jitihada za kuleta varieties nyingine kama FHIA-17 ndio zimeshikilia sekta kwa afadhari kidogo, tofauti na hapo hizo varieties za asili ziko dhaifu sana kwa hayo magonjwa.

Kwenye suala la pine trees sijawahi elewa kwanini pines zinaharibu sana mazingira na kufanya ardhi isifae kwa kilimo na hata nyasi kukauka, wakati mikoa mingine kama Njombe hazifanyi uharibifu namna ile.

Serikali pia ianzishe miradi ya nyasi za malisho kama Napier na Alfalfa. Breed ya ng'ombe wa kisasa waliochanganya na wa asili pia iletwe kwa wingi.
 
Back
Top Bottom