Webabu
JF-Expert Member
- Apr 29, 2010
- 8,870
- 14,258
Yaliyoikumba nchi ya Sudan na kuingia kwenye vita vibaya vya wenyewe kwa wenyewe sasa yameingia nchini Urusi.
Wakati nchini Sudan kulikuwa na jeshi la RSF linaloongozwa mpaka sasa na Hemedti ambapo jeshi lake linasemekana kuithibiti miji yote mitatu mikubwa ya nchi hiyo. Kule Urusi kuna jeshi la Wagner chini ya Prigozhin na ambaye amepigana sana kuzuia mashambulizi ya Ukraine.
Baada ya kujiona ana nguvu kubwa ya kijeshi ya askari 25000 wengi wakiwa ni wafungwa na kwa kujua vikosi mahiri vya Urusi viko katika vita na jeshi la Ukraine na NATO kwa ujumla, yeye ametumia fursa hiyo kufanya uasi na kudai ana ugomvi na waziri wa ulinzi Shoigu pamoja na makamanda wakuu wa Urusi. Hata hivyo katika hali ya kushangaza ameunda msafara mkubwa wa vifaru kuelekea Moscow iliko Kremlin na aliko rafiki yake wa muda mrefu Putin.
Je, ni nchi gani nyengine Ulimwenguni zenye majeshi ya kujitegemea ambayo hayako chini ya kamanda mkuu moja kwa moja. Na jee kuna haja kweli ya kufanya hivyo.Na jee Tanzania haina vikosi mfano huo wa Urusi na Sudan ?