Hatari ya machinga

Liability

Member
Joined
Oct 20, 2019
Posts
75
Reaction score
100
Kwenye swala la MACHINGA serikali inahitaji umakini mkubwa kuwatoa Hawa watu kwakuwa wamekuwa wakubwa Kama mbuyu.

Kama mnakumbuka miaka ya 2000-2015 walikuwa wanafurushwa Sana na migambo. Kuanzia mwaka 2016 mpaka sasa wamejitawala kila mahali.

Ukifika hapa Arusha Ni kero kubwa Sana. Nafikiri huu usumbufu unaweza kupunguza hata watalii.

Nashauri yafuatayo

1. Mpango wa miaka 15 uundwe ili kupunguza MACHINGA mtaani. Hii ni pamoja na kuinua sekta ya kilimo na ufugaji ili kizazi kijacho kisiangukie chote kwenye Umachinga

2. Kubadili mtaala wa elimu ili kuongeza ubunifu miongoni mwa vinana wetu

3. Serikali kutafta soko zuri kwa bidhaa za kilimo na mifugo.Pia kupunguza kodi kwa zana za kilimo na mifugo.

NB. Mbolea imepanda Bei lakni mazao ya nafaka yameshuka Bei maradufu

4. Kuapnga upya Ni kuleta vurugu . Na nawambia hili Ni gumu Sana na pengne halitawezekana kabisa. Ni bora mkatumia nguvu kubwa kuliko kusema mnapanga mpya . Hawa taenda kwasababu maeneo hayo hayana wateja na biashara Ni wateja.

NB. Tusipokuwa makini na sutala la MACHINGA tutasababisha vurugu,chuki hata rushwa kwa wale wanaopanga upya
 
Machinga wanapiga hela wanachukua mali kauli(wanapewa mzigo wanauza jioni wanarudisha na wao wanabaki na cha juu chao) wanauza hawilipi kodi ya pango wala kodi ya aina yoyote hata hivyo vitambulisho wanavyo wachache sana sasa hawa watu hata kama kungekuwa na kiwanda kila mtaa hawaendi kufanya kazi huko maana kule kwenye umachinga wanajipigia hela kiulaini.
Hakuna cha wanyonge wala nini ni wakwepa kodi tu.
 
Umetoa maoendekezo mazuri ila nakuapia hakuna kiongoz wa serikali au wabunge wa ccm wanaweza kuwaza kitu kama hicho!?? Wao hupenda hali duni za vijana ili wawe mtaji wa siasa wakati wa chaguzi!!!
 
Umetoa maoendekezo mazuri ila nakuapia hakuna kiongoz wa serikali au wabunge wa ccm wanaweza kuwaza kitu kama hicho!?? Wao hupenda hali duni za vijana ili wawe mtaji wa siasa wakati wa chaguzi!!!
umeongeaa!
 
Machinga Airlines
 
Nyie watoto wa 95 kuja juu mna makuzi sana...unafikili tatizo la machinga dar(Tanzania) limeanzia awamu ya 2015-2020??
Yeye ndio aliloli-rubberstamp....., yaani ni kama sheria ilikuwa inatungwa yeye akaja akai-sign na kuifanya ianze kutumika rasmi
 
Je kuna nchi isiyokuwa na wachuuzi?
Hata kama wapo naamini wana mahali maalum pa kufanyia uchuuzi

Kwa Arusha hata Watalii wanapungua kutokana na hii kero

Hata kupata mahali pa kukanyaga ni shida sembuse kupaki gari

HII NI KERO SANA NA INAHARIBU UTALII
 
Yeye ndio aliloli-rubberstamp....., yaani ni kama sheria ilikuwa inatungwa yeye akaja akai-sign na kuifanya ianze kutumika rasmi
Hapana,wewe ndio huna hujualo na hawa viongozi wanaotumia nguvu kuwahamisha machinga watafanikiwa kuhamisha mama ntilie na mama wauza mboga ila sio machinga.

Kwa kifupi tu machinga ni zao la sera mbovu za uingizaji wa bidhaa horela katika nchi yetu,ukosefu wa ajira kwa vijana hasa kutokuwepo kwa viwanda vya kutosha ambavyo vingetoa ajira kwa vijana mjini na vijijini,kutokuwepo na kilimo na soko la uhakika la mazao ya kilimo haya yote yanapelekea vijana wengi kukimbilia mjini kuja kuwa wachuuzi wa bidhaa ndogo ndogo kutoka nje ya nchi.

Kwa hiyo Magu aliamini kwa kuwa alijiwekeza kwenye kuanzisha miradi mikubwa mikubwa ya kimkakati ambayo kwa baadae ingeweza kutoa ajira za moja kwa moja na zisizo za moja kwamoja kwa vijana wenye ujuzi na wasio na ujuzi hivyo tatizo la machinga lingepungua kama sio kuisha kabisa.
 
Alikwambia hayo ? Kilichotokea Magu aliwaambia wafanye biashara popote na watu walipotaka kuwahamisha yeye alisema wasiondoke, dunia haiendi hivyo inabidi kuwe na utaratibu na sheria.., ndio maana nikasema hili bomu limekuwa likiendelea pole pole kipindi cha Magufuli (sio kwa kutokujua bali kwa kupiga siasa) akatumia shortcut badala ya kuanza / kujaribu kutatua tatizo akaliacha liendelee na kulifanya rasmi; kwamba kwa kuwaachia waendelee kuvunja sheria kwa kufanya kazi sehemu hatarishi ndio anawatetea

Unaongelea viwanda ? (Tupo kwenye karne ya automation na teknolojia ) unadhani viwanda vinaweza vika-absorb vijana wangapi ?, wewe ukiwa na kiwanda chako una wafanyakazi 100 mimi nina wawili na mashine zangu unategemea product ya nani itacompete sokoni....; Suluhisho la hili tatizo na sio Tanzania tu bali ulimwengu kwa ujumla ni kubadilisha our mindset (need of manpower imebadilika). Ingawa kwa nchi kama Tanzania yenye natural resources za kutosha nchi kubwa na yenye rutuba hawa machinga wangetumika kama resource / nguvu kazi na sio kero na kuachwa / kuhamasisha waendelee kufanya kazi katika maeneo hatarishi...

 
Nyie watoto wa 95 kuja juu mna makuzi sana...unafikili tatizo la machinga dar(Tanzania) limeanzia awamu ya 2015-2020??
We naee

Machinga sio tatizo
Tatizo ni kukubali uholela
Marais waliopita walipambana kurasimisha
Nani alijenga Machinga Complex?.
 
Machinga ni kundi dogo wala halitishi. Ni makosa aliyoyafanya JPM kuwaweka barabarani. Angalia Dumila amewajengea ndani ya reserve ya barabara.
Kuna siku nilikwenda Dar eneo linaitwa Mbagara ni hatari nilitembea kwa miguu kwa taabu kubwa kwani machinga wapo barabarani kabisa yaani unalazimika utembee barabarani.
Maiti haisemwi ila kosa kubwa lilifanyika
 
Wanunuzi hufuata wapi bidhaa zipo. Watu wanawafuata wamachinga kwa sababu wapo hapo. Mrundikano wa machinga karibu na maduka ni uthibitisho kuwa wanauza bidhaa za hao wenye maduka. Wakienda eneo na wasifuatwe elewa bidhaa zao zinapatikana maduka walipo kuwa, na watafute kazi ingine ya kufanya. Nguvu kazi hiyo ielekezwe kwenye uzalishaji na nchi itasonga mbele.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…