Hatari za kuchelewa kuoa

Hatari za kuchelewa kuoa

Robert Heriel Mtibeli

JF-Expert Member
Joined
Mar 24, 2018
Posts
28,297
Reaction score
68,017
HATARI ZA KUCHELEWA KUOA!

Anaandika, Robert Heriel

Hakuna umri specific wa mwanaume kuoa lakini inashauri angalau umri kuanzia miaka 25-35 ni umri sahihi Kwa kijana kupata jiko. Lakini inapendekezwa zaidi umri mzuri zaidi ni 28-31.

Ndoa itaanza kukosa umuhimu ikiwa mtu atachelewa au kuwahi kuoa.
Yaani mtu aoe anamiaka 40+ Kwa kweli hapo ni kutafuta kisukari.

Mzee mmoja mwenye Busara ninayemheshimu na ambaye ameshawahi kushika Nyadhifa kubwa mbalimbali serikalini aliwahi kuniambia; Ukiona kijana amefikisha zaidi ya miaka 33 na hajaoa basi ujue anatafuta Kuolewa"

Nilipomuuliza maana ya maneno hayo akaniambia nisubiri nitakapofikisha umri huo nitamuelewa. Kauli hiyo nimeikumbuka hivi leo baada ya kukutana na tukio lililompata moja ya marafiki zangu,

Kutupisha andiko, zifuatazo ni hatari mbaya za mwanaume kuchelewa kuoa!

1. Kumpata mwenza mwenye watoto (single mother)
Ili Jambo hili lisitokee basi itakupasa uwe umechelewa kuoa Kwa sababu ya kutafuta pesa na umezipata. Hii itakufanya uoe hata binti kigoli mwenye Bikra Lakini unamiaka sijui 37 sijui 40 alafu pesa huna alafu unatafuta kuoa. My friend hakuna atakayekuonea huruma, iwe ukweni au wanawake, zingatia wanawake hawanaga huruma na wanaume walioshiwa Step, walioishiwa mawazo, wasio na pesa.

2. Kuoa Wake za Watu, wapenzi wa watu
Hii itakufanya uwe na migogoro ya kila mara na Mkeo. Mara nyingi wanaooa Kwa kuchelewa ndio husumbuliwa Kwa kiasi kikubwa na Wake zao, na hii ni kutokana na kuwa wameoa wake za watu.

Kikawaida, mwanaume akioa akiwa Kati ya umri ya miaka 25-33 yeye ndiye humsumbua Mke wake, lakini kama ataoa akiwa na umri kuanzia miaka 36-50+ wanawake ndio huwasumbua.
Angalia ndoa nyingi ndio zipo hivyo.

3. Kuwahi Kufa mapema.
Kuchelewa kuoa mara nyingi hukivuta kifo karibu zaidi. Hii inatokana na Migogoro mipya utakayoipata Kwa Mke.

Sio ajabu mwanaume ameoa mwaka huu alafu ndani ya miaka kumi akafa.
Kwenye ndoa wanandoa wanaume waliooa muda sahihi wana-survive miaka mingi ukilinganisha na Wale wanaochelewa.

4. Kufilisika
Wanaume wengi waliochelewa kuoa wakapata maisha Fulani wengi wao hufilisika au maisha Yao kuingia katika taabu mara baada ya kuoa. Hii ni tofauti na wanaooa Kwa Wakati ambao wengi huanza Kwa maisha ya kawaida au yachini lakini kadiri siku zinavyoenda ndivyo uchumi wao unapanda. Wengi wenye maisha mazuri hivi sasa walioa katika umri sahihi Kati ya 28-33.

Sababu ya kufilisika ni kutokana na fikra za mke aliyemuoa

Kikawaida mwanamke akiolewa na Mwanaume wanaoendana kiumri katika umri wa kuoana/kuolewa, mwanamke umri wa miaka 18- 27 na Mwanaume umri wa miaka 28-33.
Mwanamke anamfikiria Mumewe Kama mwenzake, rafiki yake, na humuombea baraka Kwa Mungu.

Lakini mwanamke mwenye umri wa miaka 18-27 hawezi kuwa na fikra za kuwa Mwanaume mwenye miaka 40+ kuwa mwenzake, rafikiake, na ni ngumu kumuombea Kwa moyo wote mtu asiyemuona mwenza.

Hata mwanaume akioa mwanamke WA miaka 36 naye akiwa 40+ bado hakuna uhusiano wa kiroho hivyo masuala ya kiuchumi yataanza kuparangika.

5. Malezi ya watoto kuwa mabaya au Duni
Umri wa miaka arobaini sio wa Kulea watoto wachanga, hapo Firstborn anatakiwa awe na miaka 7-13.
Fikiria unamiaka 36 ndio unapata mtoto wa Kwanza, akili tayari imeanza kupinduka na kuwa ya utu uzima, mtoto anapaswa alelewa na Baba kijana, mtoto akishafika umri wa Balehe mzazi ndio anatakiwa awe kwenye 40+ hapo anatumia busara za utu uzima na sio ujana tena.

Baba kijana mtoto anakuwa amechangamka, bakora na ukali upo waziwazi, mtoto anajifunza Uanaume Kwa Baba kijana na sio Baba Mzee.

Wakati ambao Mkeo anakuheshimu zaidi kuliko wakati wote ni umri ukiwa kijana kuanzia miaka 28-40.
Na mtoto anatakiwa aone heshima hiyo ya mama yake kwako wewe Kama Baba katika umri huo.

Kumbuka umri wa utu uzima wanawake wanakuchukulia Kama Babu Yao😀😀

Ana uwezo wa kukutingisha.

Unajua Kwa nini wanawake wanakuheshimu na kukuogopa katika umri huu miaka 27-40? Sababu ni hizi:

I/ Una nguvu ya kutafuta maisha na pesa.

Hivyo bado wanatumaini kuwa huenda siku moja ukawa na maisha mazuri. Huko Baadaye. Ndio maana wanakustahi na kusubiri. Lakini hawezi kukuheshimu Sana katika umri wa miaka 40+ ilhali kila kitu ni dhahiri, muelekeo wa maisha yako wameshaujua, yaani umeshafika nusu ya Safari. Nguvu za mwili na Akili zimepungua, yaani Kama ullishindwa kujenga Jumba kubwa ukiwa na miaka 35 utaweza ukiwa na miaka 45?

II/ Bado unavutia na akikuacha unaweza pata mwanamke mwingine.
Wivu wa mwanamke huwa mkali kipindi hiko, wakati ukivaa nguo inakukaa, ukinyoa nywele unapendeza,
Lakini umefikisha miaka 40+ upara umechachamaa kila siku kunyoa vipara, nywele zinamvi kazi kupaka Kokoto au kunyoa kipara nani akuonee wivu. Tujiulize wanaume?

Nguo hazikai mwilini kutokana na Mabadiliko ya miili yetu, iwe kitambi au nguvu za kiume alafu utegemee heshima itabaki palepale😀 embu Acha kujidanganya.

Ni lazima uoe mwanamke ukiwa katika Enzi yako, ukiwa na nguvu, ukiwa unavaa unapendeza, ukiwa unanyoa unapendeza, ukiwa unapiga show show! Sio uoe mwanamke wakati umri umeenda wakati ambao yeye ndiye yupo kwenye Enzi yake

Zingati, saikolojia ya mtoto wa umri chini ya miaka 10 inapaswa ijengwe na Baba kijana mwenye umri chini ya 40. Zaidi ya yote unatafuta kudharauliwa na watoto wako mwenyewe. Na Dharau ya mtoto ipo miaka 2-10, umri huo mtoto huwa very Sensitive na kuwatambua wazazi au walezi wake.

Mtoto akikuheshimu katika umri huo kamwe hatakuja kukudharau akiwa mtu mzima, ipo heshima ya Baba na heshima ya Babu. Na hii yote huamuliwa na vile utakavyokuwa unaonekana na unavyo-act ukiwa nyumbani. Action za Baba kijana ni tofauti na Action za Baba mtu mzima. Sijui Kama naeleweka.

Zingatia, Malezi ya mtoto hutegemea zaidi vile Mkeo anavyokuchukulia,
Na heshima ya Mkeo kwako Inategemea na Umri na Hali yako ya kiuchumi.

Wito, Vijana mkifika umri wa kuoa Oeni, msiogope kesho msioijua, na kamwe msiisubiri na kuitumainia kesho.

Muhimu hakikisha unapata mwenza sahihi, msisubiri uchumi au kipato sahihi mungali tayari mnamwenza sahihi.

Nipumzike sasa!

Robert Heriel
Taikon wa Fasihi
Kwa sasa Dar es salaam
 
Hiyo point namba moja sio kweli, suala la kuoa mwanamke ni suala la mapenzi kwanza, then mengine yanafuata!

Unaweza kuwa kijana miaka 28 lakin mwenza wako akawa single mom na maisha yakaenda vizur kabisa,, vile vile unaweza kuwa na umri 35+ lakin ukaoa ambaye hakuwah kuzaa!

Kwa mengine sijui,, ila point ya kwanza mifano tunayo mingi Sana katika jamii yetu!
 
Kuoa ni option ya mtu. Sio kitu cha lazima. Haupungui chochote usipooa. Mjomba acha akili za kijijini huko mashambani. Kuoa ni personal sio societal.

Sijui elimu yako lakini kama ungekuwa umesoma ungeelewa suala la Ndoa sio ishu personal, ni ishu Socially, economically na political.

Kesho kutwa kwenye Sensa utaona kipengele cha Ndoa,
Ukiomba kazi lazima kwenye CV uweke Hali yako ya ndoa.

Ndoa ndio inaleta Family sijui Kama unajua hilo labda kama mwenzetu wewe ni Mnyama.

Unasema ndoa ni ishu ya Personal wakati serikali ndio inatoa vyeti vya ndoa😀😀

Faizafoxy anakuambia, huko shuleni mlienda kusomea ujinga?
 
Hiyo point namba moja sio kweli,, suala la kuoa mwanamke ni suala la mapenzi kwanza, then mengine yanafuata!

Unaweza kuwa kijana miaka 28 lakin mwenza wako akawa single mom na maisha yakaenda vizur kabisa,, vile vile unaweza kuwa na umri 35+ lakin ukaoa ambaye hakuwah kuzaa!

Kwa mengine sijui,, ila point ya kwanza mifano tunayo mingi Sana katika jamii yetu!

Huwezi kuoa single mother ukiwa na miaka 28 alafu maisha yakaenda,
Labda Kama unaota ndoto za mchana, pia labda kama huna Uelewa na Human psychology ya Mwanaume na mwanamke.

Vinginevyo uwe unazungumzia Exceptional Cases. Ambazo kwenye kila kitu ipo.
Tunachokizungumzia hapa ni Asilimia kubwa ya wanaume kulingana na nature, Hatuzungumzii Exceptional ya mtu mmoja katika ya Mia moja
 
Sijui elimu yako lakini kama ungekuwa umesoma ungeelewa suala la Ndoa sio ishu personal, ni ishu Socially, economically na political.

Kesho kutwa kwenye Sensa utaona kipengele cha Ndoa,
Ukiomba kazi lazima kwenye CV uweke Hali yako ya ndoa.

Ndoa ndio inaleta Family sijui Kama unajua hilo labda kama mwenzetu wewe ni Mnyama.

Unasema ndoa ni ishu ya Personal wakati serikali ndio inatoa vyeti vya ndoa[emoji3][emoji3]

Faizafoxy anakuambia, huko shuleni mlienda kusomea ujinga?
JF siku hizi kuna utoto mwingi saana. Bahati mbaya sana hili bandiko ni kubwa sana kwa vijana walio wengi humu JF. Ndoa ni taasisi huru kwenye jamii.
 
Sijui elimu yako lakini kama ungekuwa umesoma ungeelewa suala la Ndoa sio ishu personal, ni ishu Socially, economically na political.

Kesho kutwa kwenye Sensa utaona kipengele cha Ndoa,
Ukiomba kazi lazima kwenye CV uweke Hali yako ya ndoa.

Ndoa ndio inaleta Family sijui Kama unajua hilo labda kama mwenzetu wewe ni Mnyama.

Unasema ndoa ni ishu ya Personal wakati serikali ndio inatoa vyeti vya ndoa😀😀

Faizafoxy anakuambia, huko shuleni mlienda kusomea ujinga?
Wewe ndio mjinga kabisa. Serikali inatambua ndo lakini haikulazimishi kuoa. Ni societal pressure. Ni mkumbo. Ni trend. Binadamu mwenye akili sawasawa na thabit huwa hafati social norms, wala trends. Sawa?

Na kwa taarifa yako nimesoma kukuzidi wewe bogus unayekaa na kuandika uharo. Dunia haipo hivyo, watu hawaoi na maisha yanaenda vizuri kuliko wewe hapo na dhiki zako. Ova
 
changamoto kulazimisha ndoa - ni janga la taifa - kusubiria umpendaee ili hali nae anapendwa na mwinginee .....yabidi tuendelee kushare viungo vya uzazi. hakuna wa kwako mwenyewe

Biblia inasema, usitamani Mali ya jirani yako, wala mfanyakazi wake, wala mifugo take, wala chochote alichokuwa nacho.

Vijana wa siku hizi akiona mwenzake kaolewa naye analazimisha aolewe badala ya kusubiri wakati wake sahihi.
Matokeo yake ndio haya, kuwa na kijicho na maisha ya wengine.

Wengi hupata Depression Kwa kufananisha maisha yao na watu wengine. Dhambi
 
Biblia inasema, usitamani Mali ya jirani yako, wala mfanyakazi wake, wala mifugo take, wala chochote alichokuwa nacho.

Vijana wa siku hizi akiona mwenzake kaolewa naye analazimisha aolewe badala ya kusubiri wakati wake sahihi.
Matokeo yake ndio haya, kuwa na kijicho na maisha ya wengine.

Wengi hupata Depression Kwa kufananisha maisha yao na watu wengine. Dhambi
Nani kakwambia kila mtua anaamini au lazima aamini kwenye hiyo bibilia yako?
 
Back
Top Bottom