Haters wa JK, Kuna package yenu hapa muongeze tindikali tumboni

Haters wa JK, Kuna package yenu hapa muongeze tindikali tumboni

Dr wa Manesi

JF-Expert Member
Joined
Aug 19, 2024
Posts
6,479
Reaction score
4,974
MIAKA 18 BAADAYE: JK AKUTANA TENA NA CATHERINE, BINTI ALIYEFANYIWA UPASUAJI WA MOYO AKIWA NA MIAKA MINNE

Rais mstaafu wa Awamu ya Nne Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete, leo Mei 29, 2026 amekutana tena na Bi. Catherine P. Conrad Minja, aliyefanyiwa upasuaji wa moyo kwa mafanikio akiwa na umri wa miaka minne katika taasisi ya Muhimbili Orthopaedic Institute (MOI) miaka 18 iliyopita.

Wakati huo madaktari bingwa wa Moyo wa Taasisi ya Moyo ya JKCI walikuwa wakitumia majengo ya MOI kabla jengo lao halijakamilika.

Mara ya kwanza wawili hao walikutana Novemba 14, 2008 wakati Dkt. Kikwete akiwa Rais alipokwenda kumjulia hali Catherine hapo MOI baada ya kufanyiwa upasuaji wa moyo mapema wiki hiyo. Wakati huo Catherine alikuwa mmoja wa wagonjwa wa mwanzo kufanyiwa upasuaji huo katika taasisi hiyo.

Miaka 18 baadaye, Catherine amekua na sasa ni mwanafunzi wa mwaka wa kwanza wa Shahada ya Udaktari katika Chuo Kikuu cha Kairuki jijini Dar es salaam.

Alifika ofisini kwa Rais Mstaafu kumsabahi na kumshukuru kwa mchango wake katika kuanzisha na kuimarisha huduma za matibabu ya magonjwa ya moyo nchini.

Dkt. Kikwete alimpongeza Catherine kwa kutimiza ndoto yake ya kusomea udaktari, jambo ambalo aliahidi kulifanya alipokuwa mtoto. Alisema amefurahishwa kumuona akiwa mwenye afya njema na akijiandaa kulitumikia taifa kupitia taaluma ya tiba.

Kwa upande wake, Catherine alisema anatamani kuwa Daktari Bingwa wa Magonjwa ya Moyo ili kuwasaidia wagonjwa wenye changamoto kama aliyowahi kupitia yeye mwenyewe, akieleza kuwa hiyo itakuwa ni moja ya njia ya kumshukuru Mungu kwa zawadi ya maisha na afya njema.


Tabasamu na baraka za Binti kama huyu ndivyo vinavyofanya chuki, uzushi na Dua mbaya za haters zidunde kwa huyu jamaa. Kila haters wanavyojaribu kumzulia, kumharibia na kumuua lakini wapi.......mwamba ndo kwanza anazidi kubarikiwa. Mwenyewe Mungu nakuombea endelea kumpa moyo wa ujasiri huyo mwamba na baraka zaidi. Washushe chini, mavumbini huko, haters wake kama unavyofanya siku zote.
 
CamScanner 05-31-2026 11.56.jpg
 

Attachments

  • CamScanner 05-31-2026 11.56.jpg
    CamScanner 05-31-2026 11.56.jpg
    155.8 KB · Views: 15
Back
Top Bottom