Hati fungani ya NMB (NMB Jamii bond) kukusanya zaidi Tsh Bilioni 400

Naomba anyejua vizuri kuhusu hii Jamii bond atusaidie
 
Ngoja tuone walioweka hela huko kama yaliyomo yamo kweli!

Kule kwenye Fixed NMB ni kichefuchefu.
Huyu CEO yuko vizuri ila kwa fedha zitakapoelekezwa panatia shaka. Nanukuu:

"....ambapo fedha zote zilizopatikana kupitia Hati Fungani ya Jamii zitaelekezwa katika kutoa mikopo nafuu kwenye miradi endelevu ikiwemo miradi ya nishati mbadala, miradi ya kuzuia na kudhibiti uchafuzi wa mazingira, miradi ya maji, miradi ya kukabiliana na mabadiliko ya tabia nchi, miradi ya wanawake, vijana, elimu, afya, nyumba nafuu na mingine inayoendana na hiyo...."

Hiyo miradi niliyobold ni migumu kuleta faida kubwa kwa benki, kwa mazingira ya kibongo. Wamefanya kuenda na beat la WEF kuhusu global warming na green energy wakati ni mambo ya kina Wells Fargo na JP Morgan Chase.
 
Huenda labda wameshafanya utafiti wa kina na wameona iko fursa kwenye hilo, tuwape muda
 
Binafsi namkubali sana Bi Ruth Zaipuna,

Huyu Mama ni wa mipango sana,

Hii program anayokuja nayo italinufaisha sana Taifa hili,

Nadhani kama Taifa lazima tuvilee hivi vipaji vinavyochipukia namna hii,

Sio mbaya na NBC wakaiga hili linalofanywa na mtoto wake
 
NMB nakuamini sana, Hongera team NMB hakika mko vizuri sana
 
Wawekeze nje ya Nchi yetu pia, maana hapa Afrika Mashariki Bank za Kenya zinadominate soko la Kibenk, EQUITY BANK na KCB yapo kila mahali hapa Afrika Mashariki. CRDB, NBC na NMB zina dhima kuu ya kufanya biashara nje ya mipaka yetu.
 
Wawekeze nje ya Nchi yetu pia, maana hapa Afrika Mashariki Bank za Kenya zinadominate soko la Kibenk, EQUITY BANK na KCB yapo kila mahali hapa Afrika Mashariki. CRDB, NBC na NMB zina dhima kuu ya kufanya biashara nje ya mipaka yetu.
Sahihi kabisa, Wafungue matawi kwenye nchi zote za Africa Mashariki ili kuwapiku hao Kenya
 
Kwenye green energy wanaweza wakafanikiwa vizuri lakini serikali nayo isaidie especially kupunguza au kuondoa taxes maeneo hayo, watu wamechoka na u meme wa ovyo wa TANESCO, magari ya umeme, solar na battery technology yanaweza sana kufanikiwa TZ na itasaidia kupunguza inflation kutokana na mafuta ya waarabu tunayoagiza Kwa billions Kila mwaka, Tanzania Kuna jua kuliko mahitaji sijui kwanini solar isiwe kipaumbele, sio kwenye nyumba tuu hata viwanda vya kuzalisha panels, battery etc tujenge vyetu sio kuagiza China
 
Hakina, nakubaliana na wewe 100%

Hii bank ikiamua kuwekeza kwenye green energy naamini hata riba itapunguza sana kwani hiyo kazi itawapa pesa nyingi
 
Naona Ruth ameamua kuwanyooaha zaidi wenzake kwenye faida, hakika hii ni zaidi ya bank,

NMB ni mkombozi kubali kataa
 
Hii ni comment yangu Bora ya siku
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…