Mkuu kwa Tanzania mambo mengi yanakwamishwa na viongozi wetu. Angalia mfano wa Mabwepande ambako serikali imewagawia waathirika wa mafuriko. Kule kulikuwa na watu walioendeleza ardhi ile kwa muda mrefu na nyumba zao zimebomolewa bila kuwapa fidia. Sasa ndio maana hata mabenki yanaogopa sana hizi customary right of occupancy kwani haijapewa nguvu ya kutosha. Nadhani kuna haja ya kukipinga kifungu hichi ambacho ni discriminatory na kinazuia maendelea ya mjasiriamali.